Goli ni Goli; la Mpendazoe nalo Goli!

kwanini unafikiri mahali pekee pa kuwatetea wananchi ni Bungeni? Hivi unafikiri mipango yote ya maendeleo iliyokuwa ifanyike kishapu itaachwa kwa sababu hakuna Mbunge?

kwa kauli hii unamaanisha wabunge hawahitajiki siyo?
 
Ni nani mzigo kwa nchi kati ya ridhwani na Mpendazoe??
 
Dogo amemfuata mother kanda ya ziwa baada ya kusikia FL amenusurika kwenye ajali kule Tarime.
 
Bado mama yake naye (First lady) atatoa tamko kali zaidi kuhusu kujitoa kwa Mpendazoe CCM. Ridhiwan katoa tamko hili kama First Son. Msishangae kwa hilo, Mkimwongeza Muungwana miaka mitano atahakikisha vyeo hivyo vinapewa mamlaka kikatiba.
 

Kama vipi hoja zimekuishia unaweza kuondoka tu mwana, mie nitabakia. Sina shida na yeye na familia yake, ninachosema ni kwamba amesaliti maslahi ya wapigakura wa jimbo zima kwa sababu ya shida zake binafsi, ameshindwa kusimama kama mpiganaji kutetea hoja zake na badala yake amekimbia akalalamikie nje ya ulingo. Huu ni usaliti kwa waliomtegemea na kumwamini hadi kumchagua, na inanihusu kwa sababu mimi ni mwananchi mmojawapo ninayependa kuona mambo mazuri yanasimamiwa hadi mwisho na kitu kieleweke, siyo kuwa na mtu ambaye akitishiwa 'nyau' kidogo tu anakimbia lindo na kuwaachia hao anaowaita 'mafisadi' waendelee kujivinjari. Ametuangusha sisi wananchi. Huko alikokimbilia hataweza kuwafanya lolote hao mafisadi. Aibu kabisa kwa mtu mzima.
 

Achana na huyu Tambwe, huyu ni mchumia tumbo, mkusanya masalia ya mafisadi. Kazi yake huyu ni kama KASUKU wale wanaoogopa kuongea kwa kuhofia integrity zao wanamtumia huyu bwana kwa kiwango chake cha ku-analyse mambo kuwa kidogo mno. Anachojali yeye ni kufurahisha mabwana zake ili apate mkate wa kila siku. Ni low profile object need to be ignored. Zamani walikuwa wakimtumia "Juma Ngasongwa" kabla hajashituka
 
Ridhiwan ni mzigo kokote anakoshika nafasi! alikuwa mzigo kwenye uongozi wa Basketball yeye na Kasesela walipochaguliwa kwa mgongo na jina la Mgombea Urais wakati ule, Baba yake Kikwete, hana pointi hata chembe
 
Eti wakubwa hili haliwezi kuwa sawa na lile la Mhe. Mrema Upinzani mdomoni, CCM moyoni?
 
Mkuu BabaH, inapofikia suala la maslahi ya mtu kuguswa, familia nzima inaingia uwanjani.

Hata hii vita ya mafisadi mnayoipigia kelele, kumbukeni wana familia zao: watoto wao, kaka zao, wajomba, shangazi, na hat wanaukoo wa mbali kwani ulaji ukiingia ndani ya familia kila mtu aliyekaribu anapitiwa na ka-upepo.
 
Ni haki yake kuongea kama CCM ila ni haki yake kuondoka pia kuna wengi watakuja hapa
 

Haaaaaaaa haaaaaaaa
Kwa kweli mbavu sina kanaitwa ka-Alfan mkuu.
 
Hakuna ufalme Tanzania.Huyo Mpendazoe alichokifanya ni kuchimba kaburi lake, uhai wake kisisasa ulikiwa sawa na mgonjwa wa kansa aliyepewa siku za kuishi.Sasa hivi anajitapatapa kutumaini kwamba miujiza itatokea ili asife kisiasa.Tuone kama atapona.
 
hivi karibuni tumeona na kusikia kauli mbali mbali toka kwa viongozi wa ccm na makamanda wakimtuhumu au kusema kwamba aliye kuwa mbunge wa kishapu alikuwa ni mzigo , sasa mimi na wewe tunatakiwa tujiulize aliye mzigo ni yupi fisadi au anaye pinga ufisadi, au kwa maana nyingine ni kwamba mafisadi ndio rasilima ndani ya ccm? maana wao hawafukuzwi bali wanakumbatiwa na kubembelezwa, jingine ni hili suala la historia ya uongozi, iwe wa darasa, shule, mitaani, kazini nk.
je ccm au watu kama hao wanapenda kiongozi au mtu anaye faa awe ni mwenye historia ya uongozi uliotukuka au mtu mwadilifu au mtu mwenye historia ya uongozi uliochafuka ndio mwenye kufaa kutuongoza.
 
...Baba mtu amkanye mtoto wake akae kimya, haya mambo hayamhusu......Huyu kijana anapewa jukwaa kubwa asilostahili............
 
Ridhiwani hajui shida ya watanzania. simshangai sana kwani amekulia katika raha ya baba yake, nawashangaa hao vijana wa shinyanga wanaotoa tamko la ajabu, kumwona Mpendazoe mkosaji ni kutufanya tuamini vijana hawa wanajiandaa kuwa mafisadi wa baadae kwani huwezi kuwa na nia njema ya kuleta maendeleo ya Tanzania kupitia CCM.

CCM imeoza, tukiondoe madarakani, tunapaswa kuandaa mikakati ya kukiangusha. Tuwaunge mkono wenye nia ya dhati a kuleta maendeleo ya wananchi.

Vijana kuendelea kung'ang'ania ndani ya UVCCM ni kujilisha upepo.

CCM inahitaji miaka mingapi iweze kuleta maendeleo. miaka 33 hamna walichokkifanya.

Wanauwezo wa kusanya mabilioni kwa ajili ya uchaguzi, wakishashinda wanapunzika mpaka uchaguzi mwingine. ni ufisadi huu.

Tuamue kwa dhati
 
Huu mtaji anaowekeza sio kabisa sijui nani kamshauri nasikia ana masters ya law si angeenda kupractice kwanza badala ya kuanzisha viNGO vyake ushwara na kujishughulisha na fitna za CCM, uswahili kitu kibaya sana, Himaya inatishiwa kuvunjwa vipande lazima ang'ake!
 
Habari zenu wakuu. Wasi wasi wangu nipale wanaposema siasa ni mchezo mchafu halafu ukachezwa na familia nzima, sisi wachumia juani tutapona hapa. Nadhani siku moja utakuta chama kuanzia mwenyekiti hadi wajumbe majina yanaishia na MARIJANI halafu kura zinapatikana kama kawa maana wale mafisadi hatuwazungumzii kabisa ila mpaka wawe nje ya chama nna wasiwasi kama kuna mwendelezo wa kutimka kama Mpendazoe basi tutajua wanaobaki wanamlengo upi. Labda asitokee mwingine maana kama Mpendazoe alikua mzigo na mizigo mingine wanadai ipo sioni ni kwanini haitimuliwi mpaka kusubiri itimke yenyewe ndo mashumbulizi dhidi yao yaibuke. mizigo ipo ndugu yetu Ridhiwani kwa cheo ulichonacho ndani ya chama unaijua kama huwezi kuitimua mshauri mzee wewe ndo upo karibu kuliko sisi. Vinginevyo michango yako itakua na kasoro ndugu yetu. Kwani hizi nyufa zilianza kuonekana mapema mkawa mnazifumbia macho sasa kunabomoka mnatwambia alikua mzigo hayaingii akilini. Tuwekane sawa mkuu nakwambia hivyo sababu hata wewe ni mwanasiasa tayari ili huko mbele ukisema nawewe unataka uraisi tukuelewe kama ilivyo kwa MZEE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…