Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Tukio la kusikitisha lililotokea Desemba 25 mwaka huu siku ya sherehe za Krismasi, linamuhusisha mwanasoka mdogo mwenye umri wa miaka 14, Geral Froste kupigwa risasi na kufariki.
Imeripotiwa kwamba, risasi iliyokatisha ndoto za Geral Froste, ambaye alikuwa golikipa wa timu ya Montevideo City Torque ya nchini Uruguay ilifyatuliwa na jirani yake.
Taarifa zinabainisha kuwa Geral alikuwa muhanga wa kupigwa risasi alipojaribu kuingilia kati ugomvi uliomuhusisha mama yake katika eneo la Nuevo Ellauri huko Montevideo, Uruguay.
Katika tukio hilo, risasi ilimpiga Geral kifuani na tumboni ambapo alifariki papo hapo, licha ya juhudi za baba yake kupambana kutaka kumuwahisha hospitalini kwa matibabu.
"Tunaomboleza kifo cha Geral Froste, mlinda lango wetu wa U-14. Tunasimama bega kwa bega na familia yake, marafiki na wachezaji wenzake katika kipindi hiki cha huzuni kwetu sote. Kwaheri, Geral," imeeleza taarifa ya klabu yake.