GE2025 Golugwa awaka vikali wanachadema waliopigwa na polisi mahakamani. Endelea kuja kusikiliza kesi ya Lissu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara, Aman Golugwa akiongea na Wanahabari leo Oktoba 07, 2025 nje ya Mahakama Kuu kanda ya Dar Es Salaam amewasihi wananchi na wananchama wa chama hicho kujitokeza kusikiliza kesi inayomkabili Mwenyekiti wao wa Taifa, Tundu Lissu.

Sambamba na hilo Golugwa awaonyesha Wanahabari wananchama waliopigwa na Polisi siku ya jana Oktoba 06, 2025 wakiwa Mahakamani hapo.

Your browser is not able to display this video.
 
Serikali ya nchi hii inaongozwa na watumishi wa Ibilisi.
 
Hawa ni polisi wanaofanya matendo haya?

Hawa ni waTanzania wenzetu, wanaowafanyia unyama waTanzania wenzao kiasi hiki?

Jaji Mkuu aliposema polisi kuwepo mahakamani, hii ndiyo tafsiri ya aliyoyaagiza?

Tutamsikia tena akitolea ufafanuzi wa uwepo polisi mahakamani kwa kufanya kazi ya namna hii, au haoni umuhimu tena wa kuzungumzia swala la polisi kuwepo mahakamani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…