MBOKA NA NGAI
JF-Expert Member
- Jan 31, 2025
- 350
- 576
Leo hii, tarehe 17 Februari 2025, mjini Goma, asubuhi ya leo kumekuwa na maandamano; lengo likiwa wanajeshi wa UN waliopo Congo,hususani Goma, kwa zaidi ya miaka 20, waondoke, na kwamba usalama wao watahakikisha unatokana na wao wenyewe.
Si MOUNUSCO tu, bali na jeshi la SAMIDRC(Afrika kusini, Malawi na Tanzania). Jeshi la Burundi pia, limeombwa kufanya kila linalowezekana liondoke.
Raia hawa, wameiomba pia MONUSCO kuhakikisha wanajeshi waliokimbia vita na kupewa hifadhi kambini mwao, baada ya wenzao kujisalimisha na kupokelewa na M23, kuwaachia waliobaki na wao kuungana na wenzao, ambao kwa sasa wapo mafunzoni, kwenye kambi ya jeshi ya Rumangabo.
Wamesema,hawana imani na MONUSCO, kwa kitendo ilichofanya siku za nyuma,cha kuachia badhi yao wakiwemo wapiganaji wa kikundi cha FDLR, ili wavuruge amani mjini, huenda ikaachia na wengine tena.
Baada ya Goma kuangukia mikononi mwa M23, January 27, kwa sasa raia wanadai bora kuliko walivyokuwa wakiishi awali, na kutangaza kwamba, kwa sasa, wamehimizwa kuacha pombe kabla ya saa sita na kuwataka wafanye kazi, na wahalifu wakishughulikiwa bila huruma, jambo ambalo wanasema limegeuza hali ya usalama mjini humo, kuwa ya uhakika.