Goma: upande wa serikali wapoteza takribani watu 2500

Goma: upande wa serikali wapoteza takribani watu 2500

MBOKA NA NGAI

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2025
Posts
350
Reaction score
576
Katika zoezi linaloendelea huko mjini Goma, la kusafisha mji, shirika la msaraba mwekundu, limesema mpaka sasa zoezi la kuzika maiti zilizozagaa mjini linaendelea, na kwamba idadi ya waliokwisha zikwa imefika watu 2500(elfu mbili mia tano). Watu hawa, inasemekana ni wanajeshi wa FARDC na kundi la wazalendo. Wengi wao walipatikana kwenye magari yaliyopigwa makombola na M23, ambayo mpaka sasa yapo barabarani hayajatolewa. Shirika hilo pia limesema, bado kuna idadi ndogo inapatikana mtaani na majumbani, ya watu wanaokufa kwa majeraha walioachiwa na risasi kutokana na vita vya Goma huko. Inasemekana wengi wao wakiwa wanajeshi na wanamgambo wa wazalendo, huenda wakahofia kujikuta mikononi mwa M23;
Jana tarehe 4 Februari 2025, M23 iliongeza wanajeshi 500 mjii Goma;inasemekana ni kuongeza nguvu kukabiliana na wizi wa mida ya usiku, unaohusishwa na wanajeshi na wazalendo ambao mpaka sasa wamejificha majumbani, baada ya kuishiwa mahitaji mhimu.
Umoja wa mataifa, wenyewe umesema idadi hiyo iliyotolewa na mashilika ya misaada, si chini ya elfu 3000. Hospitali mjini zimejaa majeruhi, wengi wakiwa wanajeshi wa SADC.
Jana hiyo pia, badhi ya wanajeshi wa MONUSCO, waliruhusiwa kuingia Rwanda,wakielekea uwanja wa ndege huko Kigali ili kulejea makwao.
Kwa sasa, japokuwa raia bado hawaamini kama hiyo hali ya utulivu iliyopo Goma itaendelea, wamesema wana amani tofauti na siku za nyuma kabla M23 haijaikalia Goma.
Mpaka mdogo kati ya Rwanda na Congo umefunguliwa tena, watu wanavuka na biashara zinaendelea.

1738756363757.jpeg

1738756477336.jpeg




View: https://x.com/RDC_Times/status/1887053175636611309
 
Acha fix wewe mfuga ng'ombe apo lazma mtolewe kwa namna yoyote ile.

Peace is direct proportion with blood.
 
Propaganda kipumbavu kabisa toka kigali. Huko Goma lazima mtandikwe mrudi kwenu rwanda.
 
Duh elf mbili na mia tano si Kijiji kizima hicho
 
Back
Top Bottom