Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 276
- 473
Mimi ni Mkazi wa Gongo la Mboto Majohe, Dar es Salaam, huku kwetu kuna tatizo la uchimbaji mchanga sana, sisi Wananchi tunahofia Bonde linaweza kutanuka kutokana na uchimbaji huu
Wanaofanya hiyo kazi ya uchimbaji wamuogope Mungu, tumesharipoti katika ngazi mbalimbali za uongozi ila bado wanaendelea tu kufanya wanachokifanya ambacho ni hatari kwa usalama wa mazingira.
Inaonekana wanashirikiana na baadhi ya Wajumbe kutoka kwenye mashina yao ndio maana hawaogopi.
Mamlaka ya Mazingira wale NEMC waje huku wataona kinachoendelea, ni hatari sana.