Klamidia ni ugonjwa wa kuambukiza ambao husababishwa na bakteria zinazoitwa na sayansi kama Chlamydia trachomatis. Ugonjwa huu huwa hauonyeshi dalili za wazi kwa karibia asilimia 75 ya wanawake na asilimia 50 ya wanaume, hivyo maambukizi mengi hushindwa kufahamika mapema.
Kulingana na wakala wa afya wa Marekani (Centers for Disease Control and Prevention) ndiyo ya kwanza kati ya
maradhi ya zinaa yanayoripotiwa zaidi nchini humo: wataalamu wamekisisa kuwa karibia watu milioni tatu huambukizwa klamidia kila mwaka, lakini kulingana na CDC, ni maambukizi 660,000 tu ndiyo ambayo huripotiwa.
Watu ambao hawafahamu kuwa wameambukizwa klamidia wanaweza wasitafute tiba na hivyo wakaendelea kufanya ngono, bila ya kujua kuwa wanaeneza ugonjwa.
Wakati dalili zinapoanza kujitokeza wanaume husikia maumivu wakati wa kukojoa au kutokwa usaha katika uume. Wanawake wanaweza kutokwa damu nje ya kipindi chao, maumivu wakati wa kukojoa, kutokwa usaha katika uke, au maumivu chini ya kitovu.
Kama utaachwa bila kutibiwa katika wanawake, klamidia unaweza kuleta madhara makubwa kwa afya. Klamidia huaribu tishu za uzazi za mwanamke na kusababisha uvimbe katika fupanyonga (pelvic inflammatory disease, PID). PID inaweza kusababisha mauvimu makali sana katika fupanyonga, utasa/ugumba au utata katika ujauzito ambao unaweza kusababisha kifo.
Watoto waliozaliwa na mama waliombukizwa klamidia huwa na hatari ya kupata upofu au maambukizi katika mapafu.
Uchunguzi wa maambukizi ya klamidia hufanyika kwa kuchunguza fupanyonga na kiwango kidogo cha majimaji kutoka katika uke au uume ambayo huchunguzwa kwa uwepo wa Chlamydia trachomatis.
Uchunguzi mpya kama ule wa mkojo ili kufahamu uwepo wa bakteria wa klamidia umekuwa ukitumika pia ili kufanya uchunguzi rahisi zaidi mwa watu ambao hawaonyeshi dalili za ugonjwa.
Klamidia inatibika kwa antibaotiki.
Kisonono( Neisseria gonorrhoeae)
Kisonono ni maradhi ya zinaa ambayo husababishwa na bakteria zinazofahamika kisayansi kama Neisseria gonorrhoeae. Bakteria hizo hushambulia utandotelezi unaozunguka sehemu za siri.
Ingawa kwa makisio maambukizi 360,000 ya kisonono huripotiwa kila mwaka nchini Marekani, wataalamu wamekisia kuwa watu karibia 650,000 huambukizwa kwa mwaka.
Kama ilivyo klamidia, kisonono nayo huwa haionyeshi dalili. Kisonono ikiwepo huwa na dalili
kama zile za klamidia ambazo huhusisha mauvimu wakati wa kukojoa na kutokwa kwa maji yanayonuka au usaha katika uke au uume.
Kisonono huonekana kwa urahisi kwa wanaume ambao hutoa usaha kutoka katika mfereji wa mkojo (urethra). Huanza kidogo, lakini huongezeka na huwa mwingi na kusababisha kusikia haja ya kukojoa mara kwa mara huku kukiwa na maumivu.
Kisonono ikisambaa na kufikia prostate, mfereji wa mkojo huziba kwa kiasi fulani. Kwa wanawake maambuki hutokea katika urethra, uke au mlango wa uzazi (cervix). Ingawa mwasho unaotokana na majimaji katika uke unaweza kuwa mkubwa, mara nyingi dalili hizi huwa ni chache au hamna kabisa katika hatua za awali.
Kisonono isiyotibiwa inaweza kusababisha PID kwa wanawake. Watoto wanaozaliwa na mama wenye kisonono huwa na hatari ya kuambukizwa wakati wa kuzaliwa; maambukizo haya yanaweza kusababisha magonjwa ya meno kwa wachanga.
Uchunguzi wa ugonjwa hufanywa kwa kuchungunza usaha kutoka katika uke au uume au mkojo kwa uwepo wa Neisseria gonorrhoeae.
Kisonono iliongezeka kwa kiasi kikubwa Marekani mnamo miaka ya 1970 na mwanzoni mwa
miaka ya 1980, hadi kukaribia kufikia kiwango cha magonjwa ya mlipuko (epidemic proportions) kwa vijana wanaobalehe na watu wa umri wa kati. Kisonono hutibiwa kwa antibaotiki kadhaa, ingawa maambukizi yamekuwa na ukinzani juu ya tiba ya baadhi ya madawa katika miongo ya nyuma.
Moja kati ya mambo magumu katika kupambana na kisonono ni kutafuta mahusiano yote ya kimapenzi ya nyuma ya aliyeambukizwa ili kuweza kuzuia usambaaji zaidi wa ugonjwa.