kenge 10
JF-Expert Member
- Jul 2, 2014
- 1,450
- 2,383
Habari Wakuu,
Baada ya ban ya mifuko ya plastic, wajasiriamali wengi walichangamkia fursa ya mifuko mbadala. But mimi kama mjasiriamali pia kuna gap nililiona, kwa sababu mifuko ya plastic ilikuwa multipurpose kuanzia kubebea bidhaa, kuwashia moto uswahilini na baadhi ya abiria kutapikia au kutema mate wanaposhikwa na kichefu chefu wawapo safarini.
Gap ambalo niliona limesahaulika ni hilo la hao abiria wenye travel sickness. Basi Mzee kwa kuzingatia ile principle ya solve tatizo kwenye jamii upate hela nikajitosa Alibaba nikaagiza mzigo wa pieces 2,500 wa travel sickness bags ile inayotumika kwenye ndege na meli, na kuzingatia hapo kati pindi nasubiria mzigo uje nilizidi hamasika baada ya member humu anaeitwa TODAYS kuliongelea hili tatizo.
Mapicha picha yalianza baada ya mzigo kufika na kuanza kutafutia masoko, nilianza kuomba tender ya kusupply kwenye baadhi ya makampuni ya mabasi, but bei wanayotaka ndogo sana hii kwa sababu mpaka kufika Tanzania 1bag inacost sh. 264/- but wao wanataka kwa bei ya sh. 200/- halafu wanataka iwe na logo zao.
Nikaona sio kesi nikaacha kutafuta tender nikazama Ubungo Terminal kujaribu kuuza jumla kwa wafanyabiashara wa mule, but wakawa waoga ukizingatia wengine hawajawahi kuiona hata kwenye movie so ugeni ulichangia. Nikachage strategy nikampa jamaa mmoja mule Ubungo Terminal yeye huwapa wafanyabiashara wadogo wa mule UBT vitu kama mikate, cakes na maji kwa mali kauli then jioni wanaleta hesabu na kukata chao.
But nao pia wanasuasua sababu ya profit ndogo compared na vitu vingine wanavyouza then hii mifuko (travel sickness bags) ni migeni kwa watu wengi so inabidi watumie na muda wa kuwaelewesha wateja, mwisho wa picha inakuwa complications kwao wakati bidhaa zao wanazouza siku zote kama mikate na maji haviitaji mambo mengi.
Sasa wakuu naombeni mnishauri chochote cha kupush zaidi, maana naona kichwa kime-stuck.
Loss is a part of Game βΊ
KENGE.