Habari Wakuu.
Baada ya ban ya mifuko ya plastic, wajasiriamali wengi walichangamkia fursa ya mifuko mbadala. But mimi kama mjasiriamali pia kuna gap nililiona, kwasababu mifuko ya plastic ilikua multipurpose kuanzia kubebea bidhaa, kuwashia moto uswahilini na baadhi ya abiria kutapikia au kutema mate wanaposhikwa na kichefu chefu wawapo safarini.
Gap nililiona na kusaaulika ni hilo la hao abilia wenye travel sickness. Basi Mzee kwa kuzingatia ile principle ya solve tatizo kwenye jamii upate hela nikajitosa Alibaba nikaagiza mzigo wa pieces 2500 wa travel sickness bags ile inayotumika kwenye ndege na meli, na kuzingatia hapo kati pindi nasubiria mzigo uje nilizidi hamasika baada ya member humu anaeitwa
TODAYS kuliongelea hili tatizo.
Mapicha picha yalianza baada ya mzigo kufika na kuanza kuutafutia masoko, nilianza kuomba tender ya kusupply kwenye baadhi ya makampuni ya mabasi, but bei wanayotaka ndogo sana hii kwasababu mpaka kufika Tanzania 1bag inacost sh. 264/- but wao wanataka kwa bei ya sh. 200/- halafu wanataka iwe na logo zao.
Nikaona sio kesi nikaacha kutafuta tender nikazama Ubungo Terminal kujaribu kuuza jumla kwa wafanya biashara wa mule, but wakawa waoga ukizingatia wengine hawajawahi kuiona hata kwenye movie so ugeni ulichangia. Nikachage strategy nikampa jamaa mmoja mule Ubungo Terminal yeye huwapa wafanya biashara wadogo wa mule UBT vitu kama mikate, cakes na maji kwa mali kauli then jioni wanaleta hesabu na kukata chao.
But nao pia wanasua sua sababu ya profit ndogo compared na vitu vingine wanavyouza then hii mifuko (travel sickness bags) ni migeni kwa watu wengi so inabidi watumie na mda wa kuwaelewesha wateja, mwisho wa picha inakua complications kwao wakati bidhaa zao wanazouza siku zote kama mikate na maji haviitaji mambo mengi.
Sasa wakuu naombeni mnishauri chochote cha kupush zaidi, maana naona kichwa kimestack kubabake.
Loss is a part of Game ☺
KENGE.