Goodness of Fit: Love, Loyalty and Betrayal

Tom amepata ajali ya gari na kufariki akiwa safarini dodoma
Bwana ametoa bwana ametwaa jina la bwana libarikiwe
😂😂😂😂😂
 
Huu mwandiko naujua
Kudos mazee
 
Huezi amini jina langu baada ya hii comment yako nalo limetajwa....[emoji23][emoji23]
Tupo pamoja mkuuu
Ukipata muda tupate muendelezo wa hii series

Kwa wakina dada hata yangu ina baka jeupe ...
Namba zangu ni 0755290108[emoji23][emoji23][emoji23]
Hahahah. Hawajakutafuta mazee
 
Tom amepata ajali ya gari na kufariki akiwa safarini dodoma
Bwana ametoa bwana ametwaa jina la bwana libarikiwe
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji38][emoji38][emoji38] mkuu hebu isogeze sogeze hii stori tuendelee kufaidi.
 
Huezi amini jina langu baada ya hii comment yako nalo limetajwa....[emoji23][emoji23]
Tupo pamoja mkuuu
Ukipata muda tupate muendelezo wa hii series

Kwa wakina dada hata yangu ina baka jeupe ...
Namba zangu ni 0755290108[emoji23][emoji23][emoji23]
Jingaaa[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Episode 11: Danny the underrated!


Ok, ndugu msomaji. Najua mpaka sasa hivi mmesikia mabaya yangu tu. Najua mpaka sasa hivi mnanichukia kwa mliyoambiwa na huyo dem wa kuitwa Neema. Well, siwezi kuwalaumu. Ila kuna upande wa pili mnatakiwa kuusikiliza na kuufahamu kabla hamjaendelea kunihukumu na kunichukia. Trust me, the devil is not as terrible as he is painted!

Mimi ni mmoja kati ya watu wachache duniani wanaopenda maisha simple. Najua mmeambiwa mimi ni choka mbaya, naunga unga tu maisha eti kisa Neema kanikuta naishi chumba kimoja. Sio kama maisha yamenipiga ndugu msomaji. Nimeamua tu kuishi namna hii, sababu nakua huru zaidi. Luxury nazijua na ninazimudu nikiamua, but I just chose a simple life. You can call me an average Joe, or whatever you want. But one thing i know, is I'm doing fine!

Naitwa Daniel Rweymamu. Nimezaliwa peke yangu, nikimaanisha mtoto pekee kwa wazazi wangu. Sikupata kumfahamu baba yangu, alifariki nikiwa na miezi miwili tu. Nimelelewa na mama pekee, but i never missed anything i ever wanted as a child. Mama yangu ni msomi haswa. Alinizaa akiwa chuo alikokua anasoma na mzee wangu. Baadae akaniacha kwa bibi baada ya mzee kua amefariki, akamalizia chuo then akaingia jeshini miaka hiyo.

Mama yangu ni aina ya wale wanawake wanaopenda sana kusoma, na yuko very smart upstairs. Alimaliza chuo akiwa na first class GPA, na akaendelea kupiga kitabu hata akiwa jeshini. Amezunguka sana huko duniani kuanzia Cuba mpaka Urusi. Kaenda sana peace keeping operations za UN na AU, na amepata medali kibao za utumishi uliotukuka jeshini. Yes, huyo ndio mama yangu, Brigedia General Christina Mwaisangula. Mwanamke wa kwanza kwenye historia ya jeshi la wananchi, kufikia cheo cha brigedia. Take it or leave it, my mom is a badass!

Itoshe kusema tu kwamba mimi ndio kila kitu kwa mama yangu. Ananipenda kuliko anavyojipenda yeye. Na hapa ndipo tatizo lilipoanzia. I went to the most expensive schools kuanzia chekechea. Nilikula nilichokitaka, nilivaa nguo za bei mbaya zilizokua kwenye trend na mengineyo mengi ambayo pesa ingeweza kununua. Nilipata kila kitu, kasoro uhuru. Sikuwahi kua huru ndugu msomaji. My mom was in charge of everything. Hadi boxer zangu alininunulia yeye. She loved me a little bit too much.

Sikuruhusiwa kujichanganya mtaani. Sikua na marafiki, wala sikutakiwa kwenda popote peke yangu. Maisha yangu yalikua ni dizaini ya pembe tatu, shule - nyumbani - kanisani. I was grounded all my childhood. Rafiki zangu walikua ni wadada wa kazi, na bibi ambae tulikua tukiishi nae. Haikua tabu sana wakati niko mdogo, ila kadri nilivyozidi kukua ndivyo nilivyozidi kuona ni jinsi gani siko huru. My mom was too protective, and i didn't like it. Taratibu nikiwa sekondari, nikaanza kuruka fensi ya shule na washkaji tunaenda club then tunarudi. Taratibu nikaanza kuiona dunia ambayo awali, nilitenganishwa nayo. Na hata nyumbani pia nikaanza kua natoka, japo bi mkubwa alikua analeta utata.

Nikiwa high school, dunia ikazidi kufunguka. Nikawajua wasichana, nikazijua starehe. Nakumbuka ilikua pale Jitegemee shule ya jeshi. Hapo nikakutana na mshkaji wangu wa kuitwa Jimmy. Huyu alikua mtoto wa uswazi, na ndie aliefanya nikaifahamu mitaa ya uswahilini, kuanzia kwao Yombo mpaka kwa Aziz Ali. Hiki kipindi hadi mmea wa kijamaica nilitumia, japo sikudumu nao baada ya kuona unanizingua. Mpaka mama anakuja kushtuka ile nimerudi home baada ya kumaliza form six, it was too late. I had fallen in love with the streets.

Pamoja na hayo, mama hakuacha kunifuatilia hata nilipoingia chuo. Yani alitaka ajue kila hatua ninayopiga, niko na nani na tunafanya nini. Mbaya zaidi, aliendelea kuniwekea mipango na kufanya maamuzi yanayohusu maisha yangu bila hata kunishirikisha. I never wanted to be an engineer, ila yeye ndio alifosi. Yani hata applications za chuo alifanya yeye. Maisha yakaendelea kwa style hiyo, huku nikiwa naplan nini cha kufanya ili nipate uhuru kutoka kwa mkoloni mama yangu. On the other side, mama aliendelea kuniona mtoto tu, ambae ni lazima anisimamie kwa kila kitu bila kujali umri niliofikia.


Siku ya graduation yangu pale UDSM, ndio siku nilyofanya maamuzi magumu. Niliamua sirudi nyumbani, wala sitafanya kazi kama injinia. Wakati mama ananisubiri nyumbani alikoandaa sherehe, mimi nilikua kwenye basi naelekea Arusha. Nilizima simu na sikumuaga mtu yoyote. Nilikuja kumpigia mama simu baada ya siku tatu nikiwa Arusha. Ndugu msomaji, nilipewa kila aina ya lawama na mikwara ila haikusaidia. I had decided to move out of my mother's shadow. Sio kwamba nilimchukia, basi tu nilitaka niwe na maamuzi yangu na achievements zangu mwenyewe as a man. Nilitaka kua huru. Yakawa masaa, zikawa siku, taratibu mama akaanza kukubaliana na hali kishingo upande, influence ya bibi pia ilichangia.

Nikaanza rasmi maisha hapa Chugga nikiwa na visenti kadhaa ambavyo nilisave nikiwa chuo. Nikapanga chumba kimoja mitaa ya mianzini, nikanunua baadhi ya vitu vya muhimu. Sikutaka hata senti moja kutoka kwa bi mkubwa, sababu najua zingekuja na masharti. Nikajipa moyo kwamba mimi ni "dona kantri", sihitaji msaada wa "mabeberu" hahaaa. Wakati nikiwa bado nawaza nini cha kufanya, nikaamua kutafuta kibarua cha kujishikiza. Nikapata taarifa ya nafasi za kazi kwenye mtandao mmoja wa simu, ila walikua wanahitajika vijana kwaajili ya mauzo. Cheti changu cha uhandisi nikatia kwenye begi, nikaenda na cheti cha form six, chenye division one to be specific. To cut the story short, nikapata kibarua kwenye kitengo cha mauzo nikiwa na wengine kadhaa ambao wengi hawakua na shule kivile.

Uwezo wangu wa kujieleza na cheti changu cha form six vikafanya nikawa team leader kwenye team yangu ya mauzo. Moja ya majukumu yangu ilikua ni kufanya presentation kutoa mrejesho wa mauzo ya wiki nzima, pamoja na kuweka mipango kuhakikisha tunafikia target ya mauzo tuliyopangiwa kama team. Kwangu ilikua rahisi sana, na taratibu nikaanza kugundua nilitakiwa kusomea sales and marketing badala ya uhandisi. Niliiwezesha team yangu kufikia targets za mauzo na kuzivuka bila shida kabisa, wakati team nyingine zikisuasua.

Siku hiyo tukiwa ndani ya ukumbi wa mikutano kwaajili ya kufanya presentation ya mauzo ya wiki iliyopita, tukaambiwa tutakua na CEO mpya upande wa promotions na mauzo kanda ya kaskazini, na kitakua kikao chake cha kwanza. Team yangu ilikua imefikia target ya mauzo na kuvuka kama kawaida yetu, pia nilikua nimeandaa presentation moja nondo sana kuhusu strategy yetu ya mauzo kwa siku zijazo. Everything was on point, hatukua na wasiwasi. Huyo CEO mpya alichelewa kuja chumba cha mikutano, kwahiyo tukawa tunapiga stori tu na utani wa hapa na pale wakati tunamsubiri.


"Naitwa Neema Kingu, ni CEO mpya wa sales and promotions kwa kanda hii ya kaskazini, nimefurahi kukutana na nyinyi siku ya leo". Yalikua ni maneno ya kwanza ya CEO mpya, alipowasili kwenye chumba cha mikutano. Hii ndio siku niliyokutana na Neema kwa mara ya kwanza ndugu wasomaji.



Tukutane episode ijayo, siku isiyojulikana!
 
[emoji4][emoji4][emoji4] thanks boss. Usichoke kuipeleka hii kitu. Hadi tujue wajeda walimfanyia nn walivyoondoka nae
 
Ohoooo! Kwahiyo kanali kateka kijana wa brigedia jenearali [emoji23][emoji23][emoji23]weka mbali na watoto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…