GoodYear shamba la bibi?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kosa kubwa tulilolifanya enzi zile ni kuwaangalia watanzania wenzetu wakiyaibia mashirika yetu ya umma kama RTC, NMC, Sukari, Sukita, n.k tukidhani hayatuhusu. Baada ya mashirika yale kufa na watoto wetu kukosa ajira ndio tunaanza kulalamika.

Kampuni ya Goodyear inayouza matairi ya magari imetoa ajira kwa watanzania wenzetu na kutoa kodi, this is good for our economy. Lakini wako watanzania wenzetu wanaoshiriki ktk kuifilisi kampuni hii kwa kuiibia kiasi kikubwa cha magurudumu wanayopaswa kuyalinda na kuyatunza. Nimeshuhudia kiasi kikubwa cha magurudumu ya goodyear yakiibwa na watunza stoo na wakishirikiana na walinzi wa kampuni hii. Hii si sawa kwa ajira za wengine na uchumi wa Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…