Nachojua kuna aina mbili za piblishers.
Publishers wasafi - kwa upande wa bloggers wengi bado wapo google adsense lakini wengi wao wanacheza wanapokea laki 2 jadi laki 8 kwa mwezi, hali hii imefanya wengi kuhamia youtube kwenye nafuu, kuna kipindi youtube ilimpa millard ayo mkwaja mrefu miaka ya 2013 hadi 2015 alikuwa anapiga views kijiji ila saizi ushindani ni mkubwa na pia mabando yamepanda bei ni changamoto kiasi, pia kuna adsense ya kwenye apps nayo imetulia maana ushindani ni mdogo ukilenga penye uhitaji unaogelea pesa.
Pubishers watukutu - hawa wanatengeneza blog hata haina mpangilio inakuwa na kitufe ambacho mtu akiminya pesa imeingia, wanashare lnk za blog zao kwa kutegesha picha zinazoshawishi kuminya kwenye makundi ya facebook ili wapate watembeleaji, hawa wanapiga hadi milioni 20 kwa mwezi, adsense walipowastukia mchezo wao wakahamia propeller ads, huko nako wakazinguliwa wakahamia adsterra, kwa sasa wapo huko kunaitwa gg agency, mtu analaza dola 300 kila siku utadhani mchezo.
miaka hiyo wakiwa google adsense ikifika tarehe 22 ndio ilikuwa siku ya malipo, unakuta dogo ana miaka 19 amaenda kuchukua dola milioni 4 na upuuzi kwenye lile dirisha la kupokea hela kwa western union, hapo walikuwa wanapiga milioni 4.x kwa maksudi maana ilikuwa ukizidisha hapo basi western union inakua ngumu kutoa hela, sasa hao bloggers wakaja kufanya uchunguzi wa kuruka hicho kiunzi ndio wakajua kuna njia ya bank transfer inayorusu kutoa pesa zaidi na pesa zinaingia moja kwa moja benki, hii watu walikuwa wanapiga dola milioni 20 kila mwezi, benki pendwa ilikuwa ni Equity Bank ambayo waliweza kuungansha hio njia ya bank transfer, watu wa bank walikuwa wanashangaa sana. Mpaka sasa watu wanaendelea kupiga dollar ila wamehamia gg agency huko naskia wanalipa kwa bitcoins then unaziuza na kuzibadili ziwe tshs.
Huku mtu akikusikia anaweza kuona ni rahisi ila asikwambie mtu huku mambo yanabadilka sana, njia ikianz kutumika leo kupiga dollar unakuta inakaa miezi sita tu baada ya hapo ishachuja, hizi njia wanaziita "triki", ili kupata hizo triki inabidi uwe karibu na wenye nazo na muhimu zaidi uwe na pesa ya kulipia, triki zinauzwa mpaka milioni huko, kwa mfano kupewa orodha ya groups za kuposti link yako watu walikuwa wanauziawa laki 5, kusetiwa matangazo laki 3, n.k. na ninarudia tena, hapa inabidi uwe unajuana nao au umeshikwa mkono, unaweza kwenda na pesa wakakutolea nje.
Pia kuna visasi na umafia wa hali ya juu sana, unakuta kuna wale waliokuwa wananyimwa triki, wamepambana wakapata triki zao wakaanza kupiga dollar, hizo triki huwa hawawapi waliowanyima enzi hizo, kazi inakuwa ni kuposti tu dollar wanazopiga ila hawakupi mbinu, kuna bloggers walikuwa wanalaza dolla za kutosha miaka ya 2015 lakini baada ya triki zao kuchujaleo hii wanatia huruma uchumi umeyumba, so huku hkunaga uhakika wa kesho.
Binafsi nilikuwa natamani huko sehemu ya pili ila ilishindikana maana kuna umafia wa hali ya juu sana, nilikosai laki 3 ya kusetiwa blog, wakati naitafuta nikatonywa kwamba bado watahitaji laki 3 ya groups, sikuja tena kufikiria kurudi huko, nikaona ntamezwa tu.
Kundi la kwanza uhakika na usalama ila linahitaji uvumilivu sana maana unaweza kuanza kupiga hela ya maana kidogo baada ya msoto wa miaka mitatu. kundi la pili hilo halina uhakika na ni hatari lakini pesa ipo ukijua kucheza na game, ila ndio hivyo tena, wapo watu waliotikisa miaka ya juzi tu hapo 2018 ila leo hii wameanguka vibaya mno.