Leo kama ilivyokatika miaka yote ni siku ya Dunia. Huwa siku hii inaadhimishwa kwa kujadiliana namna gani tunaweza kuifanya dunia iendelee kuwa sehemu salama ya kuishi. Changamoto zote na namna ya kuzitatua kufuatia mabadiliko ya tabia nchi.
Nimefarijika kuona mlima Kilimanjaro leo utafahamiaka kwa watumia google kote duniani, japo kuwa leo utafahamika zaidi kwa jinsi tulivyoshindwa kuutunza.
Picha inayoonekana leo ni ulinganifu wa kiwango cha barafu kwa miaka tofauti kwa mwezi Dec kutokea mwaka 1986-2020. Picha hiyo ikionyesha kuwa barafu imepungua kwa asilimia kubwa.
Kama taifa tunapitia mambo mengi ya kimazingira na utunzaji wa uoto wa asili. Picha hii imenifanya niwaze kuhusu sakata la Ngorongoro. Ni kiasi gani shughuli za kibinadamu katika eneo lile zinavyoadhiri maisha ya wanyama na uoto wa asili?
Je, tusubiri baada ya miaka ishirini tuwekewe picha ya jinsi Ngorongoro ilivyokuwa hapo kabla na jinsi itakavyokuwa? Pakiwa na ng'ombe na mbuzi badala ya nyumbu na swala?
Picha hii itupe funzo la namna gani tusipokuwa makini kizazi kijacho kitakosa fursa za kiuchumi kwa kutoweka kwa vivutio mbalimbali