Google imeanza kuweka sehemu ya Magic Eraser kwa watumiaji wa iOS (iPhone)

Google imeanza kuweka sehemu ya Magic Eraser kwa watumiaji wa iOS (iPhone)

Apollo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2011
Posts
4,920
Reaction score
3,240
Android 14 attery copy.jpg
Google imeanza kuweka uwezo wa kufuta vitu na watu kwenye picha. Kwa kawaida feature hii inapatikana bure kwa watumiaji wa Google Pixels 6 na Google Pixel 7.

Kwa wiki hii Google imeanza kuweka feature hii bure kwa watumiaji wa iOS ambao wanalipia huduma ya Google One. Huduma hii ya Google One huwa inapatikana kwa watumiaji wanaolipia Storage ya ziada na inakuwa na features za ziada kama vile Google VPN.

Hivyo Google itaanza kuhitaji Dola 1.99 kwa mwezi ili kupaa feature hii. Ila kwa watumiaji wa Google Pixel wanaipata Bure. Ila kwa 1.99$ haina VPN, ili kupata Google VPN inaanza kwa 9.99$.

Sio vyema kwa sababu ilitakiwa ipatikane bure kwa watumiaji wote wa Androids. Kwa sasa kuna apps nyingi tayari zinatumia feature hii ila Google ina uwezo mzuri wa kufuta vitu na watu kwenye picha. Ila inaweka huduma hii iwe ya kulipia na kulazimisha watumiaji kununua Google Pixels ili kupata upendeleo lakini ilipaswa iwe available kwa watumiaji wote wa Androids 13 na kuendelea.

Google imeanza kuweka sehemu ya Magic Eraser kwa watumiaji wa iOS (iPhone)
 
Back
Top Bottom