Google pixel Fold Haitoki tena

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391

Kutoka katika vyanzo vya kusambaza material na utengenezaji wa simu za Google Pixels, kwa supply na order za sasa, inaonekana Google imefanya maamuzi ya kusitisha kuzitengeneza simu za Pixel Fold ambazo zilitegemewa kutoka mwaka huu.

Mabadiliko hayo yatapelekea Pixel Fold isitoke mwisho wa mwaka huu na mwanzo wa mwaka 2022. Labda inaweza kutoka mwisho wa mwaka 2022 lakini sio hivi karibuni.

Pixel Fold ilitegemewa itakuwa kama Galaxy Z Fold ya Samsung japo katika muundo haitakuwa na kamera kama Pixel 6 Pro. Ilitegemewa itakuwa na kioo ambacho unaweza kuikunja kama kitabu, unaweza kuitumia kama simu na unaweza kunitumia kama tablet/pad.

Labda imeona ni mapema sana kuanza kushindana na soko la Folding Phones kama Galaxy, Xiaomi na Huawei. Pia dunia ipo katika shortage ya semiconductors na brands nyingi za simu hazipati suppy on time. Google imeamua kusitisha ili kuangalia soko la simu linavyoenda na itaisaidia kukuza soko la Pixel 6 kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…