Google waichonganisha Tanzania na Malawi, ramani yao yaonyesha ziwa Nyasa lote la Malawi, Wizara ya Elimu Tanzania yatoa onyo kwa mashule yote

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Mabeberu naona kama wanawashwa washwa, kupitia shirika lao la kibeberu, wametoa ramani inayoonyesha eti ziwa lote ni mali ya Malawi.

Hongera Wizara ya Elimu kwa kutoa muongozo. Tunasubiri Wizara ya Mambo ya nje ipeleke official complaint kwa hawa nyamaume.
 
Attachments

"Wanafiki wanataka tuingie vitani, wanatuchonganisha ili tuje tupigane baadae waseme vita vya panzi furaha kwa kunguru!."

maneno hayo aliropoka mlevi mmoja akiwa chakali tilalila!.
 
Hii Ishu Kipindi chá Joyce Banda JK wa Msoga aliizima Naona inaibuliwa kivingine
 
Nyie vilaza wa CCM tulieni.
Rasilimali zenye thamani ya Quadrillions of dollars mmeshindwa kuzitumia lakini mnataka kila kitu kiwe chenu.
Lake nyasa ni mali halali ya Malawi
 
Mabeberu naona kama wanawashwa washwa, kupitia shirika lao la kibeberu, wametoa ramani inayoonyesha eti ziwa lote ni mali ya Malawi.

Hongera Wizara ya Elimu kwa kutoa muongozo. Tunasubiri Wizara ya Mambo ya nje ipeleke official complaint kwa hawa nyamaume.
Hakuna wakati ambao Ziwa Malawi halijawahi kuwa la Malawi. Dunia nzima inalitambua kama Ziwa Malawi na lipo nchini Malawi ni Tanzania pekee ambao tunalitambua kama ziwa Nyasa na ramani zetu zinaonyesha mpaka umepita katkati ya Ziwa.
Ingawa kwa logic , Tanzania ipo sahihi, haiwezekani mpaka wa ziwa uwe pale linapoishia ziwa.
Ziwa ni rasilimali inayopaswa kutumiwa na viumbe wote waliopo wote waliopo eneo lile haiwezekani wananchi wa Matema na Mbmba bay wakatazwe kutumia ziwa kwa madai eti ni la Malawi.
 
Watu unaosema wanawachonganisha wanawapa hado msaada wa mchele tena kwenye mji mkuu wa nchi.

Idiot.
images - 2024-12-18T183711.965.jpeg
 
Hakuna wakati ambao Ziwa Malawi halijawahi kuwa la Malawi. Dunia nzima inalitambua kama Ziwa Malawi na lipo nchini Malawi ni Tanzania pekee ambao tunalitambua kama ziwa Nyasa na ramani zetu zinaonyesha mpaka umepita katkati ya Ziwa.
Ingawa kwa logic , Tanzania ipo sahihi, haiwezekani mpaka wa ziwa uwe pale linapoishia ziwa.
Ziwa ni rasilimali inayopaswa kutumiwa na viumbe wote waliopo wote waliopo eneo lile haiwezekani wananchi wa Matema na Mbmba bay wakatazwe kutumia ziwa kwa madai eti ni la Malawi.
Tanzania tuko sahihi, kwa mfano ziwa Nyasa likitanuka kwa kilomita 100, jamaa watasema hayo maji bado ni mpaka?
 
Mabeberu naona kama wanawashwa washwa, kupitia shirika lao la kibeberu, wametoa ramani inayoonyesha eti ziwa lote ni mali ya Malawi.

Hongera Wizara ya Elimu kwa kutoa muongozo. Tunasubiri Wizara ya Mambo ya nje ipeleke official complaint kwa hawa nyamaume.
Mbona muongozo unapwaya? Hizo ramani ziko wapi? Walishindwa nini kuzi~annex?
 
Mabeberu naona kama wanawashwa washwa, kupitia shirika lao la kibeberu, wametoa ramani inayoonyesha eti ziwa lote ni mali ya Malawi.

Hongera Wizara ya Elimu kwa kutoa muongozo. Tunasubiri Wizara ya Mambo ya nje ipeleke official complaint kwa hawa nyamaume.
Mwaka 2016 tulikuwa kwenye mkutano mmoja Ujerumani, presenter mmoja aliambiwa na KM tuliyeongozana naye kwenye hiyo session aondoe ramani ya Tanzania kwenye PPT kwa hofu kuwa ingezua gumzo kubwa kwakuwa ramani ile ilionyesha mpaka umepita katikati ya ziwa Nyasa
 
Tanzania tuko sahihi, kwa mfano ziwa Nyasa likitanuka kwa kilomita 100, jamaa watasema hayo maji bado ni mpaka?
Hujaelewa kitu.
Jamaa amekwambia mipaka ya kisheria kimataifa ndio inavyosema hivyo, mpaka hauko katikati ya ziwa, lakini hilo sio haki. Sasa ni jukumu la Tanzania kupambana kisheria hilo libadilike.
 
Back
Top Bottom