Kang
JF-Expert Member
- Jun 24, 2008
- 5,655
- 2,506
Google wametangaza maboresho ya kupunguza wizi na kulinda data pale simu inapoibiwa. Baadhi zitakuja na Android 15 na baadhi zitakuja kwenye Android kuanzia 10 kwa kupitia update ya Play.
Android’s theft protection features keep your device and data safe
Android’s theft protection features keep your device and data safe
- Theft Detection Lock Simu itatumia AI kujua kama imapokonywa na kujifunga yenyewe, simu itajua kama imepokonywa mkononi na mtu kukimbia nayo ambapo itajilock yenyewe.
- Offline Device Lock Simu itajilock yenyewe kama mwizi akijaribu kuiweka offline kwa kipindi kirefu, kuzima data ni moja ya mbinu za wezi ili usiweze kutumia Find My Device au kuifuta simu remotely so sasa simu itajilock yeneywe kama iko offline kipindi kirefu.
- Factory Reset Protection ambayo ipo sasa tayari imeboreshwa hii inazuia simu kutumika baada ya kufanyiwa factory reset, inabidi uweke gmail account ya mwenye simu kabla ya kuweza kutumia, hapa ni kujaribu kupunguza mauzo ya simu zilizoibiwa so unaweza kuuza kama spea tu.
- Uwezo wa kuficha apps nyuma ya PIN/biometrics, so unaweza kuficha app zenye data private zaidi kama za benki, hii nadhani kuna apps unaweza kuinstall kufanya kitu kama hiki ila sasa itakuwa imo ndani ya Android.
- Setting za kuzima Find My device, screen timeout sasa zitahitaji PIN/biometrics. So mtu akishika simu yako wakati ipo unlocked hawezi kuzima Find My Device wala kuongeza muda wa timeout bila PIN.
- Kubadili baadhi ya settings kama Find My Device sasa kutahitaji biometrics hata kama unajua PIN kama uko location isiyotambulika, so simu inaongeza ulinzi kama ipo location isiyoijua.
- Remote Lock unaweza kuilock simu yako kwa kutumia namba yake tu na neno la siri, hii ni kama Find My Device ila haihitaji kulogin na google acount maana wengi hawajui password zao.