Gospel Music Kibiashara

Matendo Andrew

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2014
Posts
748
Reaction score
367
Wadau mimi kwa majina ni Matendo Andrew ni Gospel singer, lakini hapa nimekuja kama Manager wa Matendo Andrew. Nahitaji mtu au kampuni nifanye nayo kazi, kazi ni hii hapa. Nimesha record album yenye nyimbo 18 audio na video album ina nyimbo 8.

Nipo na rafiki yangu fulani ambae nilimshawishi kufanya nae biashara hii yaani mimi nilitoa mawazo ya hii biashara na yeye nikamshawishi awekeze pesa, tumefanikiwa kurecord kama nilivyo sema hapo juu, lakini nilipo mshawishi tuandike mkataba wa makubaliano juu ya ku share huku ali sua sua mpaka leo sijui kwa nini.

Nyimbo zipo radio na tv, baadhi, na COSSOTA nimesha sajili, nikaandaa bajeji ya uzinduzi na kopi za kuanzia biashara yetu nikampa tukakubaliana tutazindua kabla ya Pasaka, lakini naona siku zimeisha na hakuna chochote kinacho endelea. Japo napata tetesi kwamba hali yake kifedha sio nzuri kwa sasa.

Sasa wadau mimi hii ndio nilisha ianza na kwamba itakua ndio kazi yangu japo nina proffesion nyingine, nashindwa kuendelea mbele kwasababu yeye ndio alikua muwezeshaji wa mambo yote ili mwisho wa siku tufanye biashara hii vizuri na kwa faida najua mnajua ilivyo na maslai ikifanywa vyema. Sasa mimi nahisi huyu rafiki yangu alikua ananisaidia tuu kuinua huduma yangu ya uimbaji na sio na yeye kuhitaji kutengeneza faida.

Sasa nimepata wazo la kutafuta mtu mzoefu wa biashara hii, tukutane akague bidhaa hii, aangalie jinsi gani itaingia sokoni halafu mimi nita mkutanisha na mwekezaji wa mwanzo ili wawe wame share bidhaa iende sokoni, na tutapanga jinsi gani biashara itafanyika.

Kwa kifupi saana ndio hivyo, angalia video mbili youtube kwa kuandika Matendo Andrew Usinipite na Matendo Andrew Ndani ya yesu, au tembelea http://matendomgeni.blogspot.com/ usikilize baadhi ya nyimbo au nicheck whatsup kwa 0759 83 93 10 nikutumie audio na tuwasiliane zaidi kwa 0714 04 50 80.

ASANTE.

 
Mbona maelezo ya upande wa pili hatutayajua ,unaelekea huna uhakika ni nini kumempata mdau wako .Ili kuwa na uhakika kwanini usiongee naye kabla ya kufikia hatua uliyoamua badala ya kuhisi tu.
 
As ante kyalosangi lakini nimesha omba saana kukaa nae kujadili mwendelezo huu hanipi time. Yupo bize saana name hanipi ahadi yeyote nisaidieni mawazo kabla walimwengu hawaja nishauri vbaya kuna watu walisha nishauri niiuze kimyakmya.ASANTE
 
Unafanya Gospel kama business
Usiweke sanaa mbele pesa kwakua ni kosa nyimbo za Mungu as businesses
 
As ante kyalosangi lakini nimesha omba saana kukaa nae kujadili mwendelezo huu hanipi time. Yupo bize saana name hanipi ahadi yeyote nisaidieni mawazo kabla walimwengu hawaja nishauri vbaya kuna watu walisha nishauri niiuze kimyakmya.ASANTE
Kma ndivyo we endelea watafute watu kama Msama,Mbogo na wengineo uongeenao ,aidhaa pata uzoefu kwa wanamuziki wenzio usijwe ingizwa chaka na Wadosi
 
Nilipo jua kwamba nina kitu Mungu kanipa nilikifanyia kazi na naamini kila
mtu ako na kitu amepewa na Mungu ili kimpe maisha bora. kufanya Mziki
wa injili ukiwa pia ni mnyenyekevu mbele za aliye kupa kipawa hicho naona
sio tatizo, naamini pia ya kwamba Mungu anawachukia wote wasio na vipato
eti wakisingizia Mungu hajataka wao wawe na maisha bora wakati wamepewa vitu
vya kuwafanya wawe na maisha bora. hivi unataka mtu atumie mil 20 kufanya mziki
wa injili halafu atoe buree usikilize kwako? au una maana gani kusema ni kosa?
 

Shame upon you! unafanya gospel kibiashara? Ushindwe na Ulegee . Am tellin you hautafika MBALI, na utazimwa kama KIBATARI! Gospel ya ukweli ipo Roman Catholic, KKKT, ANGLICAN na AIC coz wao wanafanya gospel kwa ajili ya kumtangaza Mungu, sio nyie makanjanja wa kaliba yako, mnaofanya gospel kwa sababu za kibiashara.
 
Kwa bahati mbaya hizo ulizo taja zoote ni kwaya na hari zao
kiuchumi siku zote hua si nzuri saana pamoja na kazi zao nzuuri wanazo fanya
umewahi kujiuliza kwa nini? Kumbuka kua Mungu hapendezwi na hari zetu mbaya
kiuchumi wakati ametupatia material ambapo kubadilisha kua bidhaa ni juhudi
yako mwanadamu alijua tukiwa kama wanyama hatutaweza akatupatia UTASHI
huo ndio utusaidie kujua lipi jema na lipi baya, kwahiyo wewe unatamani turecord nyimbo
tusikilize wenyewe? hebu umefika wakati tuache unafiki na roho za wivu naamini hapo
ulipo una album za waimbaji binafsi au unampenda mwimbaji binafsi, sasa bila juhudi binafsi
angefika hapo alipo mpaka unampenda? hata hivyo ubarikiwe kwa mchango wako nimekuelewa
ila sito regea kwa unyenyekevu nitamwimbia Mungu huku niki muomba akupeleke dukani ukanunue
album yangu itakayo kua na nyimbo 18 halafu kwa bei ya tsh 4000 tuu, ASANTE
 
Unafanya Gospel kama business
Usiweke sanaa mbele pesa kwakua ni kosa nyimbo za Mungu as businesses

We nae! nanikakuambia kuwa hizo ni nyimbo za Mungu?. hizo ni nyimbo za Disko mambo yesu.
 
hakuna cha RC,KKT wala cha AIC. Ote hao wanapiga mziki, hawamuimbii Mungu.
 
Wakati ule wa zamani wakati hawa mitume na manabii wetu kina mwingira wakiwa masela tu nyimbo zilitumika kueneza injili sehemu ambazo ukristo haukuwa umeimarika na waimbaji hawakuangalia maslahi kwanza waliimba kumtumikia Mungu. Enzi hizi kumeinuka sijui ni roho wa aina gani ambapo tofauti ya nyimbo ya Injili na mnazoziita za kidunia ni pale litajwapo jina la bwana tu ila kwenye mauzo na maslahi ni kama kina Roma Mkatoliki tu na waimbaji wengi wangependa hata kutoga masikio kama kina Diamond sema ni wigo tu umewabana!
 

Album zao wanagawa bure?
 

angalia vizuri reasoning yako, hiyo comment yako juu ya kwaya haijaeleweka. kwaya ndiyo msingi wa nyimbo zote za dini. anyway, what do i know!
 
hakuna cha RC,KKT wala cha AIC. Ote hao wanapiga mziki, hawamuimbii Mungu.

Nahisi nimekumbana na wewe mahali fulani...Nafikiri jukwaa la elimu kule ambapo wale wahuni wa Mwenge University waliofukuzwa kwakugomea mitihan....

Hebu nikumbushe ndio wewe..??
 
Hakuna ilipo halalishwa huduma ya kimungu upewe bure japo sisi tunatoa bure hivi unajua thamani ya muZiki na unav yo andaliwa? Ukiwa mbishi kuwezi kujifunza Mimi najua kwa mwenye roho mbya hata ukimpa DVD bure ataivunja mbele yako then atanunua kwa hela
Kisilisili ili usijue kama anapenda kaz yako.
 
Shalom! Naomba nikwambie kitu hapa, hakuna injili ya bure kweli na kila mtumishi atakula ktk madhabahu yake. Madhabahu unayotumika wewe ni ipi? Nafikiri mentor aliyekulea na kukufunza alitaka ukue kwanza kiroho ndio kazi yako itaweza kukulipa maadam unakazi nyingine ulipaswa kutumika ktk madhabahu yako hata ukipokea tuzo ndogo hadi kanisa/waumini waione karama yako ndio utahitajika na kulipwa. Uko kujitoa kwa mwalimu wako ndio unakutana na haya. Kwavile ushasema unataka iwe biashara basi peleka kwa kina Msama au producer wengine. Vinginevyo tulia imba kanisani kwako na kwa wakati wako utajapokea riziki yako. Watoto wa Asafu na hata mfalme Daudi walikuwa na kipaji cha kuimba na walilipwa ktk madhabahu yao, chagua moja.
 
Unafanya Gospel kama business
Usiweke sanaa mbele pesa kwakua ni kosa nyimbo za Mungu as businesses

Kuimba kwake Gospel kama kunawafanya watu waburudike na kumkumbuka Mungu.., who cares..

au would you rather afanye biashara ndio achangie mambo ya mungu ? (ya Kaisari asimwachie Kaisari)..,

Kila mtu ana mchango wake mkuu, yeye anaburudisha na Kumsifu Mungu as well as kujipati kipato yeye na familia yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…