poposindege
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 453
- 175
[h=2]Nyota wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Ujerumani, Mario Gotze amesema kuwa ni vigumu kwa mchezaji mwingine yeyote kufikia hatua ambayo Lionel Messi yupo kwa sasa.[/h]Katika kumsifia nyota huyo wa Argentina na Barcelona, Gotze aliwaambia waandishi wa habari wa Ujerumani kuwa Messi amefikia mafanikio makubwa katika kazi yake ya mpira na kwamba hatua aliopo iko juu sana na hadhani kuwa kama kuna mtu yeyote awezae kuifika ngazi aliyopo.
Gotze ambaye aliifunga Timu ya Argentina bao la ushindi katika mechi ya fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2014, alisema kuwa utendaji wa messi hivi karibuni umeongezeka maradufu. "Baadhi ya mechi unaweza kucheza kwa kiwango, lakini ni vigumu sana kuendelea na utendaji huo kila mechi" alisema.
Messi ambaye amechukua mara nne zawadi ya Ballon d'Orr, mpaka sasa amefunga magoli 34 na kasaidia katika ufungaji wa mabao 20 katika mechi 32 alizocheza.