Govt: We goofed on 1.85bn/- deal


Huu mradi unanikumbusha ule wa Maktaba ya Taifa. Mwekezaji ( Raha Towers) alipewa kibali kuongeza ghorofa juu ya maktaba kwa makubaliano ili kuwaongezea kipato Maktaba. Kilichotokea ni jengo kuharibiwa kimandhari (maoni yangu binafsi) na maktaba kupoteza matumizi ya lift, na kupewa kiofisi uchochoroni kwenye ghorofa mpya. Sehemu kubwa ya parking ya mbele ikachukuliwa na mwekezaji ambaye hakuwa nayo (chache zilizokuwepo aliishazigeuza ofisi) kwenye jengo lake lililojirani. Kwa kifupi, maktaba walikula hasara na jamii kubwa zaidi maana maktaba ( kwa wenzetu ni sehemu muhimu sana katika jamii) haijaweza kurudi kwenye enzi zake za miaka ya sabini. Vile vile jiji letu likapoteza moja ya majengo machache ambayo tungeweza kujivunia.

Huyu jamaa hajasema hizo square metre 1300 zitakuwa wapi na zitakuwa na facilities gani! Watapewa parking kiasi gani? Watachangia kiasi gani kwenye gharama za kuendesha jengo ( ulinzi, usafi wa mazingira, ukarabati wa jengo n.k.) na nani atakayeamua gharama hizi n.k.? Wamesema, at least 1300, bila kuainisha nani atakayeamua kiasi kamili. Hivi hii ina maana serikali wataweza kudai hata mara kumi ya hizi? Kuna maswali mengi ambayo yanastahili majibu.

Huyu jamaa amelenga kwenye hizo ghorofa za maofisi. Hivi kweli huu ni wakati wa kuongeza idadi ya watu watakaokuwa wanaingia na kutoka katikati ya jiji kila siku? Tuna infrastructure ya kubeba hili? Kwa nini serikali ya jiji isifungue CBD nyingine ambako maghorofa kama haya yatajengwa baada ya kuwekeza kwenye infrastructure? Master Plan ya jiji inasema nini kuhusu hili? Mkurugunzi wa mambo ya Kale anasema nini kuhusu effect kwenye mandhari ya kihistoria ya jiji?

Hilo la soko la almasi ni danganya toto! haliingii kichwani kama ilivyokuwa Tancut!
 
Tancut? Labda umechanganya, nimeongelea TANSORT.

Ndio, what am talking about hali ingiliani na hili la kiwanja. It's probably meant for a whole new thread.

Nilikua nasema tu kwamba yale yote walio wazushia TANSORT wakati ule, chanzo chote jibu linapatikana kwenye pale nimeku-qoute. I know it is out of this topic but I could not resist maanake sidhani kama hile issue ilieleweka vizuri judging by wengi nilio ongea nao.
 

Mkuu, nilikuwa nazungumzia kakampuni kakukata almasi kalilkokuwa Iringa na kalikuwa kanaitwa Tancut kama sijakosea.

You are absolutely right kuwa hii issue ya Tansort. Ni uozo mtupu na ninashangaa kwa nini halijachangamkiwa. Uko sasa hihi tena kwa unganisha hii international auction centre na hiyo ofisi ya London ambako wauzaji wetu wa almasi inaelekea wanalipa royalties. Inatisha ndugu yangu.


 
Kama juhudi zake za mwanzo zilikumbana na ukuta inakuwaje disgraced PM atoe maagizo ili huyu so called mwekezaji kupata hilo eneo?????????
 

Ndio, was not talking about Tancut ambayo ilikua ni shirika la umma ambalo lilisha filisiwa zamani ile.

Nilikua naongelea hio TANSORT ambayo ilikua formed enzi za 60s kwasababu Nyerere alijua kwamba kuuza diamonds zetu, tunaitaji kuchakarika nao huko huko kweye Diamond Markets kupata bei nzuri na ku-deal na hawa yatu at a level playing field. Na kama ulivyosema, you cannot have a diamond market kwenye hizi nchi zetu masikini na kufikiria kwamba mtu atakufwata bongo nakukupa bei nzuri.

Hao TANSORT wanalipwa hio royalty kutoka kwa De Beers kwa diamonds walizo zitoa TZ na kuzikagua kutizama bei ambayo zinaweza ku fetch according to the markets huko huko kusudi TZ ipate due share inzuri nakuto tapeliwa.

Na hio complain kwenye paste nikisingizio tu na tricks za hio kampuni kuhusu high running cost of electricity bla bla. Ni trick kama hizo zilizo tuingiza wabongo enzi zile mpaka tumefikia kwenye 25% ownership. Selekali had a 50 50 share of ownership kabla yakuuza 25% yake to make De Beers majority shareholder sasa. Wali-claim mgodi auna kitu na kwamba auingizi kitu and they are ready to go, afalu baada ya mda hapo wakauziwa 25% ya selekali kwa bei ya njugu utacheka. Sasa wako 75%, making all decisions nakuchimba mi-diamonds mingi wakati before wali-claim there is nothing there. Hii ya high running cost ni ku-dodge wasilipe what is due to the government, the usual abuses ya hizi mining companies.

Na bado walitaka kuing'oa hile TANSORT kule London, ata kwa kile kidogo inayo collect kule kusidi they should have total control. You are right, haya mambo ya madini yanatisha. Ngoja tungojee ripoti zao hizi tuone wanasema nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…