GOZI LA NG'OMBE : Ozil; Sindano ya nguo kwenye ubao

iddy eba

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2015
Posts
573
Reaction score
1,171
By Nicasius Agwanda

Katika ubongo wa mpenda soka yeyote,
katika fikra za binadamu
anayeufahamu mchezo huu na kwenye
macho ya mtu anayesisimka kila
anapotazama soka ambayo ndio
inayoongoza kwa kupendwa duniani,
kuna viungo wachache duniani
wabunifu wanaomzidi Mesut Ozil.
Ndio, Ozil huyu mwenye damu ya
Kituruki aliyeamua kuishi na
kujifungia ndani ya ukuta wa Berlin na
kuukacha mji wa Ankara. Ni huyu
ambaye ameishi miaka 27 huku miguu
yake ikiwa inatazama kwa usahihi
zaidi kuliko macho yake makubwa.
Kiungo ambaye wengi wanaamini
anaweza kuishi na Elias Maguli na
wote tukaamini kuwa kipaji chake
hakina tofauti kubwa na Thomas
Muller wa Bayern Munich.
Ni huyu ambaye Wenger na dunia
tuliamini kuwa Real Madrid
hawakumtendea haki na
hawakuheshimu kile ambacho Mungu
alimjaalia pale walipoamua kumfanya
ampishe mchezaji Isco, ile siku ambayo
Florentino Perez alipomvua rasmi jezi
yake namba 10 na Wenger akaaminika
kuokota tunda jangwani. Katika dunia
hii ya soka ambayo pesa zake zinanuka
hakukuwa na namna nyingine zaidi ya
Wenger kuamua kuacha asili yake na
hakuna ambaye aliona amepungukiwa
akili, akafungua pochi yake yenye
kufuli na akapeleka fedha pale
Bernabeu, akatizama miwani ya Perez
kisha akamwambia nipe dhahabu
nikapambe jengo langu pale Emirates.
Jengo ambalo lilikosa vito vyenye
thamani muda mrefu baada ya Wenger
kuamua kuishi akiamini kuwa anaweza
kutumia mgodi wake mwenyewe
kuzalisha vito vinavyopatikana
kwingine.
Hii ilikuwa ni mwanzo tu wa mpango
mpya wa kifedha chini ya Wenger
ambao baadaye ulimhusisha Alexis
Sanchez kabla haujasogea mpaka
kufika kwa Granit Xhaka ambaye
anapenda rangi nyekundu ya waamuzi
na Shokdrani Mustaffi, tofali
inayojaribu kuimarisha ukuta kwenye
eneo la ulinzi la Arsenal. Hii
ilionekana kuwa ndio ufalme mpya
ambao unafika ndani ya Emirates,
tabia mpya ya Wenger katika maisha
yake na kila kitu kilionekana kwenda
sawa na kuwa katika mtiririko sahihi.
Ni Ozil huyu ambaye alimfanya kila
mchezaji kuwa bora msimu
uliomalizika hasa wakati ambao
mchezaji Alexis Sanchez akiwa
majeruhi.
Ni Ozil huyu ambaye mwaka jana
wakati kama huu tayari alikuwa
kapiga pasi 16 za mabao na akawa
amejivika ufalme katika kila
analofanya.
Maisha siku zote hayafanani, soka
linabadilika, na mbinu kiuchezaji
zinakuwa tofauti kila kukicha. Maisha
haya ya Ozil yalifanikiwa wakati
Sanchez akicheza kutokea pembeni, na
mara nyingi yeye ndiye aliyetumika
kama kiunganishi na roho ya Arsenal
katika kuamua nini kinatakiwa kutokea
baadae. Wakati yeye anafikiri
kuendelea kuwa yule, Wenger alikuwa
anafikiri tofauti, Wenger alikuwa
anaamini tofauti. Kwenye akili ya
Wenger kulikuwa na Arsenal ambayo
inatakiwa kucheza kwa uhuru zaidi
kutoka katika eneo la kiungo mpaka
eneo la ushambuliaji. Kwenye mawazo
ya Wenger, kulikuwa na Arsenal
ambayo ingeruhusu kila mchezaji
auguse mpira kabla ya goli, kila
mchezaji awe karibu na eneo la adui ili
kutoa nafasi ya wachezaji tofauti kuwa
na uwezo wa kufunga hivyo kujenga
tabia ya kutokutabirika na ambayo
ingewafanya kuwa hatari zaidi.
Hii ilimaanisha hata Ozil mwenyewe
alitakiwa aanze kufunga badala ya
kufikiri zaidi kutoa pasi za mwisho,
kipaji ambacho hakujaaliwa nacho
kabla, ndio Ozil hajawahi kuwa
mfungaji mzuri. Lakini pia hii
ilimaanisha kuwa Arsenal ingeweza
kutumia wachezaji wafupi kikosini na
kumfanya Alex Sanchez kuwa mchezaji
wao muhimu zaidi na mshambuliaji wa
mwisho hivyo kutoka kwenye uwiano
ulizoeleka kati yake na Ozil. Arsenal
ikahamia kwa Sanchez, inacheza
kupitia yeye na kwa sababu ni
mchezaji anayekuwa bora zaidi akiwa
na mpira miguuni kwake ilimaanisha
kuwa Ozil anakuwa katika wakati
mgumu zaidi kwa sababu muda
mwingi anakuwa mbali na tukio ama
anakosa mpira kwenye mguu wake wa
kushoto ili atizame eneo la kupeleka
mpira ambalo binadamu wa kawaida
angehitaji darubini kugundua kuwa
kulikuwa na nafasi ya kupenyeza
mpira na ukapita.
Uamuzi huu wa Wenger ulikuwa na
umuhimu kwa Arsenal kwa ujumla
lakini mfumo wowote mpya lazima
unufaishe baadhi na uumize wengine.
Huu wa Arsenal uliwafanya kuwa
imara zaidi kama timu, ukawapa
nafasi ya kuwa na mbadala au kuwa
na chaguo la pili pindi ambapo
unagoma kupitia kwa Olivier Giroud
ambaye alizoeleka kuanza na sasa
anatokea benchi muda mwingi. Bahati
mbaya ni kuwa mhanga katika hili
alitakiwa kuwa Ozil, huyu majukumu
yake yalibadilika na kwa sababu
hakupata nafasi tena ya kuwa na
mpira muda mwingi ilimaanisha kuwa
kazi yake kubwa kwa sasa ni kutumika
kwanza kuhusishanisha eneo la kiungo
wa ukabaji na eneo la ushambuliaji
huku akijifunza kufunga zaidi. Hii
tafsiri yake pana zaidi ni kuwa Ozil
alitakiwa atoke katika nafasi za mbele
za gari ili Sanchez ajitawale na ashike
usukani vyema. Tatizo pekee katika
mabadiliko haya ni kuwa uhitaji
mchezaji kuwa huru zaidi kuweza
kuvaa uhusika tofauti na aliuzoea.
Ozil hakuzoea tabia hizi, hakukuzwa
hivi na wala hakuwahi kuishi ili afanye
kazi hii. Maisha yake yalikuwa
kuwafanya washambuliaji wafurahi,
yeye magoli kwake hayana umuhimu
mkubwa kama pasi za magoli na ndio
maisha ambayo hata wakati wa ukuaji
wake wa soka akiwa na Real Madrid
ndivyo yalivyokuwa. Alikuwa tayari
kuwafanya Ronaldo na Benzema
waione pepo kwa urahisi zaidi na wao
walifurahi alichokifanya. Walimpa
mpira miguuni kwake muda mwingi na
wakakimbia kwenye nafasi sahihi ili
atumie vipimo vyake vya uhandisi
kuwatafuta na siku zote aliwafikia.
Ozil ni mchezaji mwenye kipaji
kikubwa, kipaji cha kipee lakini ni
kipaji ambacho kinaweza kuathirika
kwa kiasi kikubwa kutokana na namna
soka linavyobadilika kila kukicha.
Kumtaka akae kwenye maeneo ya
kufunga muda mwingi kwake ni tusi,
kumyang’anya mpira miguuni kwake
ni unyanyasaji, unamnyima
anachokipenda. Kuna aina ya
wachezaji wanaoweza kubadilika
haraka katika mitindo hii lakini sio
Ozil, na maisha yalivyo sio muda
mrefu anaweza kulia kwa kukosa
furaha. Kipaji chake ni cha kipekee, ni
nadra kukipata lakini ni rahisi
kuathirika kama ilivyo sasa. Bahati
mbaya zaidi ni kuwa Sanchez
amekuwa mwanaume na anafanya kila
lililokuwa sahihi. Ozil ni sindano pale
unapotaka aunganishe nguo, lakini
hawezi kuunga ubao, ni ngumu kwake.
Labda tuendelee kumvumilia, ila
mfumo huu sio rafiki.
 
utamuona kwa hull city ni mkali sana au wale ludogorets
 
VDUME WA CHEC WALMBANA MBAV NA SANCHEZ NAE KABANWA. UCHAMBUZ WAKO MZUR MKUU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…