Mjadala wa Richmond unashika kasi sasa .Grace Kiwelu akitoa hoja bungeni amesema anaomba wote walio tajwa na kujiuzuru ili kuepusha wao kukimbia Nchi na wapelekwe Mahakamani na pia amemshauri Lowasa kama ameona hajatendewa haki aende Makahamani ndiko haki na kila kitu kitasikika .
Kazi kubwa Keenja kasimama anatetea hoja ni ya CCM na wapinzani waachane nayo .Keenja anaongea sasa .
Mkuu Lunyungu,
ebu tufafanulie alikuwa anamaanisha nini, maana hayo maneno yanakatisha tamaa kweli kweli.
Inaonekana anakerwa sana na upinzani.
Lunyungu
wana mpango gani na RA na Yona maana waliidharau kamati kwa kukataa kuhojiwa na mwanahalisi wamesema kamati ilidokezwa na Salva kuwa richmond ni ya RA.
Hakuna aliyeanza kuwashika bango?
Kazi kubwa Keenja kasimama anatetea hoja ni ya CCM na wapinzani waachane nayo .Keenja anaongea sasa .
Shukrani Lunyungu
endelea kutuhabarisha yanayojiri hapo Dom
Huyo babu sasa naona akili zake zimechakaa vibaya!.......... Narudia, ni mpumbavu na anapaswa kupuuzwa! Kaniudhi sana. (Mtoto wake Elia alikuwa mwanafunzi wangu, akiisoma post hii aniwie radhi tu, nimeshindwa kuvumilia!)
Huyo babu sasa naona akili zake zimechakaa vibaya! Anamaanisha CCM wakitoa hoja wapinzani hawaruhusiwi kuchangia? Kama hivyo basi wangeitoa katika kikao ambacho wapinzani huwa hawahudhurii, huko kwenye mikutano ya CCM huko! Si adabu kutamka maneno yasiyofaa kwa mzee, lakini kwa uzee wa aina ya Keenja ni sahihi kabisa kumwita mpumbavu! Anasahau kuwa hiyo hoja ni ya Kamati Teule ya Bunge ambayo Mwenyekiti wake Mwakyembe aliisoma siku kadhaa nyuma? Au anataka kutudanganya kuwa ile Kamati teule ya Bunge ni ya CCM. Narudia, ni mpumbavu na anapaswa kupuuzwa! Kaniudhi sana. (Mtoto wake Elia alikuwa mwanafunzi wangu, akiisoma post hii aniwie radhi tu, nimeshindwa kuvumilia!)