Graduates: Kuna cha kujifunza hapa, nilianza na laki 3 sasa nina mtaji wa laki 8 ndani ya miezi 10


Mkuu nilipomaliza chuo niliajiriwa..bahati nzuri taluma yangu ina soko kubwa,so sikuona haja ya kufanya shughuli nyingine na hata hivyo ninatumika sana kazini..sasa bi mkubwa aliniambia anafikiria kufungua duka pale nyumbani.Nilipopiga hesabu za faida ya kwenye kiberiti,sabuni za kipande,pipi nk..ni tsh 50,100,ikienda sana ni 1000 nk. niliona ni biashara kichaa..kwa kuangalia faida za namna hiyo niliona kabisa hata kulipia frem itakuwa mtihani..nilipolinganisha na salary yangu,nikamwambia,mke wangu subiri kwanza..lengo langu lilikuwa nimkatishe tamaa ili aachane na wazo lile..maana niliona kama that was too low kwa level yangu!

Mwaka uliofuata nikapata nafasi ya kwenda shule kujiendeleza kielimu..nilipoondoka tu bibie akachonga na mwenye nyumba wakakubaliana..akamwita fundi akaja akagawa sehemu ya sebule,akaweka frem! Kisha akaniambia ule mpango wake wa duka hakuufuta ila kwa kuwa mimi ndio nilikuwa namwekea kauzibe na sasa nimeondoka,basi akaanza utekelezaji..sikukubaliana sana naye ila nilimwacha aanze ili akikwama nimzodoe kwa kuwa alikataa ushauri wangu wa kisomi!!

Nakumbuka alianza na tsh laki 4..tena wakati anaanza kibanda chake kilikuwa ni kati ya vile vidogo kabisa..na kama mnavyojua,wateja wengi wananunua bidhaa kwenye maduka yanayoonekana yamejaa sana..kwa hiyo kwa siku alikuwa anauza kati 20,000 hadi 50,000..yeye alikuwa anafungasha kwenye waduka ya jumla ya pale karibu ambayo wamiliki wake walikuwa wananifahamu kutokana na kazi yangu..kwa hiyo walikuwa wanamwamini na kumpatia mzigo anakuja anauza kisha anarudisha hela..

Nilipoona anaendelea,nikaanza kuvutiwa,niliporudi nyumbani likizo nikachukua mkopo benki nikampa 2mil akaongeza kwenye mtaji..baada ya miezi 6 akaanza kuuza vitu kwa jumla na reja reja..hapa kulikuwa na changamoto..kwa kawaida kuuza vitu kwa jumla faida inapungua,so unategemea zaidi mzunguko wa biashara..ukiwa na mzunguko mzuri ndo faida inaonekana..

Mwanzo wa wazo la kuuza jumla lilikuwa kufanya biashara na wenye frem wenzetu wa hapa kwetu..lakini haikuwa hivyo..pamoja na kwamba tulikuwa na vitu vingi vya muhimu lakini hawakupenda kuja kufungasha kwetu..walikuwa tayari kwenda mjini tena bila kujali kwamba gharama ni kubwa kuliko kama wangefungashia kwetu..bibie alikuwa anaongea na wengine anawaambia wachukue mzigo wakauze na kurejesha hela kama alivyoanza yeye,lakini bahati mbaya walikuwa hawaonekani tena baada ya hapo!

Baada ya kuona kama tunauza sana,kuna watu watatu nao walifungua maduka ya jumla hapa hapa..wakawa wanauza bidhaa zama tunazouza..ushindani ukawa mkubwa mauzo yakashuka..tukaendelea kumwomba mungu..lakini haikupita miezi 6 biashara ikawashinda wengine wakafunga kabisa na wengine wanauza tu kwa reja reja..

Kiufupi,pamoja na kumfanyia mtima nyongo,gharama na maisha yangu ya shule yaliendeshwa na biashara ya bi mkubwa..kwa sasa mtaji wa duka lake ni zaidi ya 50mil..ana duka dogo la nguo,amejenga,kuna viwanja na mashamba kadhaa na mimi binafsi nina mishe zangu ninazoendesha;vyote hivyo si kwa sababu ya mshahara wangu,bali kutokana na bisashara za bi mkubwa..nasema hivi kwa sababu mshahara wangu hautoshi hata kulipia ada ya watoto,chakula na maisha ya familia ya kila siku.

Nilichojifunza ni kwamba,spirit ya ujasiriamali mtu anazaliwa nayo..huku ukubwani tunaiga tu na ndio maana wengi tunafeli..na hasa kwa hawa tunaojiita wasomi ndo kabisaa..maana tunapoanza tunataka tufanikiwe kesho;kitu ambacho hakiwezekani..vile vile wasomi hawapendi ku'take' risk..mtu anafikiria zaidi hasara badala ya faida ndogo ya kuanzia..

Pili,ni uaminifu..watu wengi wanasema wafanya biashara wakubwa si waaminifu;kwa maana kwamba waliofanikiwa wamefanya hivyo kwa kudhulumu wengine..ila mimi nasema kama unaanza,hakuna namna utafanikiwa bila kuwa mwaminifu..ukishaaminiwa,huo ni mtaji namba moja..bi mkuwa ametoka kwa sababu walikuwa wanamwamini wanampa mzigo anakuja anauza na kurejesha pesa ya watu..ila kuna wale aliokuwa anawaamini,anawapa mzigo,wakiondoka hawarudi tena..mpaka leo wako palepale na wanatia aibu kweli..

 

ongera wengne kina #nifah wanasubir haya wafanyiwe na chama
 

Kuna funzo hapa kiukweli watu tunakata tamaa mapema
 
Hongera kwa uthubutu.

Nina imani ukifumbua macho utaona fursa mingine mingi zinazoendana na shughuli unayoifanya. Ukiweza jiwekee malengo yanayoendana na muda,kwani hiyo itakubana uhakikishe unayatimiza ndani ya muda husika.

Wawekee pia na kagenge kadogo kwani nako kanalipa na mtaji wake ni mdogo sana.

Kila lakheri
 
Kuna funzo hapa kiukweli watu tunakata tamaa mapema

Tatizo kubwa ni kukosa akili ya ubunifu..unaweza ukaona mtu amefungua biashara yake,ukaona kama inamlipa sana..kisha unafungua biashara kama ile ili ikulipe kama yeye;tena unafungua hapo pembeni yake..unasahau kuwa kilichoongezeka hapo ni bidhaa tu,lakini wateja ni wale wale,so itabidi mgawane hawa wateja,na kwa vyovyote vile hutauza kama yeye..na pengine kwa kuwa yeye tayari ana wateja wake ambao huwezi kujua anafanya vipi nao biashara,atauza zaidi yako..mwisho wa siku utaishia kupata stress tu za bure,maana ulichotegemea haijaenda kama ulivyopanga..

 

Jana nilipost hapa kutaka kupata ushauri lakini naona kama watu bado wanatafakari..nilitaka kuanza kufuga au kulima ila bado naendelea kufanya utafiti katika mazingira haya..

Pia last week nilipost hapa kuomba walimu ambao wapo comitted tufanye nao kazi..walijitokeza wengi..ila wengi wao hawakuwa serious..kuna ambao tunaendelea na mazunguzo na kama tutaelewana tutafanya kazi..

Ila kiukweli kupitia kwa bi mkubwa nimejifunza mambo makubwa sana juu ya ujasiriamali..sometimes naona kama ajira yangu ni kikwazo..ila kifupi kuna fursa nyingi sana lakini mimi kwa upande wangu kikwazo kikubwa ni muda na usimamizi..maana biashara yoyote inayoanza unatakiwa kuisimamia wewe mwenyewe kwa 100% vinginevyo ukimweka mtu,ndani ya miezi 6 tu,kwisha habari yake..

 
 
Hongereni kwa kutia moyo wajasiliamali mliothubutu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…