Graduates wengi (61%) wa Tanzania hawana sifa za kuajiriwa!

Graduates wengi (61%) wa Tanzania hawana sifa za kuajiriwa!

Mwanamayu

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2010
Posts
11,662
Reaction score
6,888
Hivi haya matatizo yanatokea wapi? Kukosa juhudi binafsi za mwanafunzi au ni systemic?! Kwa sababu kwenye maofisi mengi ni kama kinachosemwa kwenye huu utafiti ni kweli. Je, yaliyosemwa kwenye utafiti huu hayaendani na tabia ya baadhi ya wafanyakazi wenzio?!

Source: IPPMedia Home
 
utakuaje na sifa uku kazi nyingi wanataka uzoefu mika 2 na kuendelea na wewe graduate uo uzoefu utaupata wapi?
 
Shida iko primary na secondary. . . . .walimu wasiposikilizwa na kutendewa kwa stahiki zao. . . . .zitafanywa kila jitihada kuanzia kubadili viwango vya ufaulu mpaka mfumo wa kuingia vyuoni!

Ukijikwaa usikimbilie kufuta vumbi ila hangaika na sababu ya kujikwaa kwako!!!
 
!
!
utafiti huo ni wa kweli sana. Graduates wengi walikuwa wako deep katika kujibu maswali by the time wanasoma wakitegemea the same itahappen kazini. Kazini hakuna maswali wala marks, hakuna course work. Ni application ya skills and knowledge katika kutatua matatizo yanayobadilika kila saa. Aisee
 
M
shida iko primary na secondary. . . . .walimu wasiposikilizwa na kutendewa kwa stahiki zao. . . . .zitafanywa kila jitihada kuanzia kubadili viwango vya ufaulu mpaka mfumo wa kuingia vyuoni!

Ukijikwaa usikimbilie kufuta vumbi ila hangaika na sababu ya kujikwaa kwako!!!

mkuu uko sahihi sana.elimu yetu inaendeshwa kisiasa .si vema kuboresha paa la nyumba kwenye msingi wa barafu.nchi nyingi wanajali walimu wao wa msingi na sekondari kwetu tuna kazi ya kuwadharau na kuwabeza. Kwani hao graduates sio product ya walimu wa shule za msingi? Sasa watakuwaje safi ikiwa msingi huku chini ni mbovu? Tusipoligundua hilo tutamtafuta mchawi hatutampata.
 
Mfumo wenyewe hamuandai mtu kuweza kuwa competent rather than craming.
 
Kunahaja ya kupitia upya mitaala yetu,mitaala yetu kwakiasi kikubwa anachokisoma mwanafunzi sio kile anachoenda kukifanya mtaani au kazini,hali hii imejitokeza mpaka vyuo vikuu kuna baadhi ya course ni majina tu lakini hazimuandai mwanafunzi kupambana na uhalisia uliopo mtaani au kazini
 
Kigezo cha uzoefu ndio pingamizi kwa wengi wetu.sasa mtu nmemaliza degree unakuta nafit qualification zooote ila tatizo lipo kweny uzoefu!!uzoefu miaka 3,,5,,9 mi ntaupata wapi sasa wakati nlkua shule kuhakikisha ufaulu wa hali ya juu??icho kitu kinaniboaa sanaa!!
 
Back
Top Bottom