Graduates wengi tunapitia wakati mgumu sana, sema jamii inaona kama hatujielewi

jooohs

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2017
Posts
2,524
Reaction score
10,287
Unajua kuna msemo unasema ndege mjanja hunasa kwenye tundu bovu, ndio graduates wengi ambao hatuna kazi tunapitia hiyo hali yaani hatuna haki kabisa, now tumekuwa jalala la matusi sii la Saba, fm4 failure, waliobahatika kupata vijikazi, wanatuona kama wajinga, wazazi jamii inayotuzunguka wote wanatuona mafala hakuna wakututetea.

Yaani ukitaka kuiona dunia chungu, maliza masomo/degree halafu usipate sehemu ya kujishikiza au mchongo wowote asee utachekwa hadi na watoto wadogo, najua wengi hasa graduate mnanielewa ninacho zungumzia, just imagine interview ya jana TRA watu wanaitwa zaidi ya elfu sita kugombania nafasi mbili kwa kweli inasikitisha.

Now hata nafasi za kujitolea kwenye makampuni hazipo yaani ebu fikiria mtu anajitoa kufanya kazi bila malipo lakini bado unakataliwa, sio tu kwenye makampuni makubwa, hata kufanya kazi kama kibarua kwenye miradi ya ujenzi napo bilabila, viwanda vidogo vya kufyatua tofali unakuta kumejaa.

Yaani kwa sasa mambo yamebana hata nafasi ya kufanya field ukiwa bado unasoma napo unaweza kukosa kabisa, kuna zile kazi za kupakua mizigo inayotoka mikoani kama magunia ya mpunga, viazi huko kote bila connection hata kama una phd dalali hakupi kazi.

Kilicho nisukuma niandike haya yote leo kuna jamaa yangu ninapokaa ametimuliwa na mama mwenye nyumba kisa kushindwa kulipa kodi. Jamaa yeye ni graduate wa ba education toka 2018 anauza matunda kwa wanafunzi wa chuo kwao ni Kigoma kisa Corona mambo yameenda vibaya kodi yake iliisha toka tarehe moja leo mama mwenye nyumba ameleta dalali wakakagua nyumba na vitu viko ndani akafukuzwa.

Jambo ambalo nataka kuwaambia magraduate wenzangu usikomalie tu kukaa Dar es Salaam ukiona maisha hayaeleweki rudisha mpira kwa kipa sio kukomaa kwenye hakuna, mikoani kuna fursa nyingi kuliko Dar es Salaam kwanini nasema hivyo, Dar es Salaam imeshakamatwa na wafanyabiashara wakubwa.

Waliobaki wengi ni machinga kama unataka kuamini nenda kesho Kariakoo, Ilala, Makumbusho, Gongo la mboto ujionee mwenyewe machinga walivyojazana.

Kuingia kwenye system ya kujiajiri hasa biashara ni rahisi sana kwa mji unaokua mfano Dodoma kuliko sehemu kama Dar es salaam ambayo tayari mabeberu walishaishika toka kitambo, jaribu kuangalia gharama za ulipaji pango, umeme, usafiri ndio utaelewa.

Yaani kodi tu ya fremu Dar sehemu ya uchochoroni unaambiwa laki 4 na dalali anataka ya mwezi mmoja,

Najua kuna madogo wengi watasoma hapa, nakwambia kabisa jaribu kutafuta ujuzi binafsi huko chini, ukiona kitabu hakipandi nenda veta, kasomee electronics/ ufundi simu, gerage/umeme wa magari, pikipiki, ufundi bomba, umeme majumbani, kupaka rangi, kutengeneza furniture/sofa hawa watu wana uhakika wa kuishi mjini vizuri kuliko graduate wa kwenye makaratasi.

Kariakoo pale kuna mtu ana masters nilimkuta anafundishwa kutengeneza simu na fm4 B tena pale kwenye msururu wa vile vimeza vilivyopangana pale njee, maisha yamempiga hatari,

Nihitimishe tu kwa kusema Mungu atujaalie na atutangulie tuweze kutimiza ndoto zetu na atuwezeshe kuvuka salama katika hiki kipindi cha mpito.
 
Ulichosema ni kweli kabisa Teknolojia na ongezeko la watu limesababisha uhaba wa ajira na hii inatupa picha kuwa tuendako tatizo linazidi kuwa kubwa kuliko ilivyo sasa.

Ila Basic needs za maisha ziko tatu Food, Clothes na Shelter nachotaka kusema ni kuwa hii nchi bado ina maeneo makubwa especially vijijini tena kwa bei rahisi pointi ya msingi ni kuwa Mali tutaipata shambani tulime kwa ajili ya chakula excess tufanye biashara ila tuweze kumudu gharama nyingine za maisha.
 
Mkuu unajua kweli maana ya motivation speaker?? Au unaandika tu kisa umejisikia .kama hujaelewa mada pita kushoto
 
Andiko zuri mkuu, ni kweli kung'ang'ania dar ni shida zaidi maana unaingia katika utumwa ambao sio rahisi kutoka......Kukosa ajira nilipitia kwa kipindi kifupi miezi miwili tu ila niliteseka sana na kujifunza kitu kikubwa sana maishani......chamsingi ni kumuomva Mungu afungue milango ya baraka na kuwa na nidhamu ya matumizi....
 
Nikweli mkuu. Sijalaumu mtu, au taasisi yoyote, ila nimejaribu kuelezea hali halisi wengi tunayo kutananayo .
Mkuu huu ushauri ni wamuhimu sana kwa graduate maana mimi nilifikiri mbali sana nikajaribu hadi saidia fundi huko usiku unalala mdomo wazi viungo vinauma usingizi hauji .....nashukuru Mungu aliniwezesha nikapata ajira ila bila hiyo ajira ingekuwa kazi maana kuna kipindi unaangalia mbele unaona giza......

Sikuhizi ninanidhamu sana ya matumizi ya pesa naogopa sana kustruggle tena na vibiashara ninavyoweza fanya huwa navifanya pia....
 
Nimepita hali hiyo 2016-2018, ni hali ngumu asikwambie mtu. Mzee anakupigia simu anauliza unafanya nini mjini rudi nyumbani uje kuvuna, maza nae anakupiga spana mpaka unazima simu hupokei simu za wazee.
Ila Dar kuzuri aise asikwambie mtu. Ukichanga karata vizuri lazima utusue.
 
Kufukuzwa kwenye nyumba kwa huyo Graduate mmoja ndio kunakufanya utapike mambo yote haya ?

Ninyi ndio kina Magufulu, hampendi challenges kwenye maisha yenu. Changamoto mnaona kama Jehannum,
Inavyoonekana wewe ni katai ya wanaoiogopa mno Dar kiasi kwamba unamtisha hapa kila mtu.

Mimi niwashauri Graduates, Dar ndio Silicon Valley ya Tanzania. Ni nkji unaoakutaka kufikiria, kama huwezi kufikiria Dar itakushinda,

Binafsi siogopi kulala njaa, kulala nje wala kunyeshewa mvua.

Kama wewe ukilala njaa siku moja unaona ukojela, rudi kwa wadogo zako nyumbani.
 
Ndio mkuu, unajua kabla hujapata tatizo la ajira, akili huwa nzito kufunguka. Lakin ukifika mtaani baada ya kumaliza masomo, ajira hakuna, ukianza kuzunguka mtaani nakuona mafundi waliotoka veta kila siku wako kazini wanapiga mzigo ndio akili hurudi sawa nakujua ulikosea mahali kwenye kufanya chaguzi
 
Hakika mkuu.
 
Kweli mkuu ni kumuomba Mungu. Hapo kwenye gharama za matumizi dar es salaam ni kubwa mno. Saving inakuwa tabu mno ukuchukua gharama za kodi ya nyumba, maji,umeme,uchafu, usafiri, chakula, hubaki hata na kitu mfukoni
 
Graduate mimi ningekubaliwa kupata chimbo pale upanga ningekuwa na uwezo wa kutusi ajira zote duniani aisee.
[emoji23][emoji23] unamillion ya kulipa pango kwa mwezi. Achilia mbali upatikanaji wa nafasi
 
Mkuu katoe maono yako kwenye uzi wangu.
 
Mkuu elimu ya kwenye makaratasi isikuchanganye, huyo mmoja nimetolea tu mfano. Matatizo mengine sio mpaka ufanye sampling ndio upate accurate results yanaonekana kwa macho. Hivi ukiwa na kuku mia ukakuta mmoja kati Yao ni mgonjwa utafanya nini?

Pia kwenye andiko langu sijaongelea maswala ya kushinda njaa hayo unajua ulikoyatoa.

Pia hakuna sehemu nimelazimisha mtu aondoke dar arudi mkoani,
Mimi nilichokuwa na maanisha kunaurahisi wa kuanzisha biashara kwenye miji inayoendelea mfano dodoma/iringa kuliko dar, kwa kuangalia gharama za kodi ya fremu, umeme, chumba cha kukaa, usafiri, upatikanaji wa location nzuri ya biashara. Hapa na zungumzia graduate ambae mtaji wake ni wakawaida sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…