Graphs za Maisha: Kupanda, kushuka na kuwa uniform

Graphs za Maisha: Kupanda, kushuka na kuwa uniform

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
GRAPHS ZA MAISHA: KUPANDA, KUSHUKA NA KÛWA UNIFORM​

Anaandika, Robert Heriel Mtibeli

Maisha ni hesabu ya 📉 📈 Graph. Maisha ni safari. Katika safari kûna nyakati, mazîngira, na wahusika àmbao huweza kuathiri Graphy yako.

Wàpo waliozaliwa katika Maisha àmbayo Graphy zào zîpo juu. Zimepanda. Maisha mazuri, huduma na mahitaji yôte muhimu na anasa walizikuta. Wàpo Maisha Yao yanaendelea kuwa Hukohuko juu mpaka wanamaliza safari ya Maisha Yao Duniani. Hawa NI wachache Mno.

Kuna wale waliozaliwa Maisha yakiwa juu lakini baadaye wakashuka. Kûna wale walianzia juu wakashuka Kisha wakarudi juu. Alafu kûna lile kundi kûbwa àmbalo walianzia CHINI na bado wàpo CHINI.

Unapoishi katika ulimwengu huu. Lazima ujue kuwa hutobaki hivyohivyo Siku zote. Kûna kupanda na KUSHUKA, na nadra Sana kuwa uniform. Leo upo hivi Kesho utakuwa vile. Upo chini Kesho unaweza kuwa juu. Au Leo upo juu Kesho siô ajabu ukawa CHINI.

Kuanguka NI sehemu ya Maisha. Kupanda ni sehemu ya Maisha kijana na Binti yàngu. Usijichanganye.

MAMBO YA KUFANYA GRAPH YA MAISHA YAKO INAPOSHUKA AU IKIWA CHINI

1. Elewa upo Wakati gàni na usijaribu kufurukuta

Ni muhimu kutambua kuwa upo katika KUSHUKA, hii itakusaidia pakubwa. Usifurukute, just relax
Usitake kuonyesha Watu kuwa bado upo juu, au usitake kuwa-prove watu kuwa haupo CHINI.
Usifurukute.

Be Calm
Mfano ulikuwa unasomesha Watoto Shule za gharama (kulipia) mara ghafla mambo yakakubadilikia, usifurukute, sijui uchukue mikopo, sijui uuze Mali, nop! Tulia. Au Mchumba kakumwaga, usitaka kuthibitisha chochote Kwa yeyote kwamba bado unamvuto. Usijiingize kwèñye mahusiano Mengine harakaharaka kutaka kuthibitisha Jambo Fulani. Utapigwa.

Kwèñye Kanuni ya Vita, endapo ikatokea umepigwa au kushambuliwa na Adui hasa Kwa njia ya Ambush, yàani shambulio la kushtukiza. Usitake mapambano au kuonyesha uwezo wako ilhali hujajipanga. NI Vizuri kukimbia na kutulia ukajipanga

2. Punguza yasiyo na umuhimu (Pukutisha Majani kama Mti Wakati wa Kiangazi)
Ukiwa katika anguko au upo down au umeshuka kimaisha ni vizuri kupunguza mahitaji yasiyo na ulazima. Kupunguza wahusika wasio na ulazima. Kwèñye mshuko usilete Kiburi cha kutaka kuwa juu. Hata kwèñye udereva, gari kwèñye mshuko wa kilima na konakona hupunguza mwendo.

3. Tumia Muda mwingi ukiwa pekeeako kujipa Muda wa kutafakari
Ukiwa kwèñye anguko haishauriwi kutafuta washauri shauri au watoa Msaada. Muda mwingi utumie kuwa mwenyewe ukijitafakari na kutafakari nini ufanye ujisaidie mwenyewe. Elewa, kisosholojia Wanyama akiwemo binadamu hutumia anguko la Wengine kujinufaisha na kukumaliza Kabisa. Ni rahisi kuhujumiwa na Watu ukiwa down na kumalizwa Kabisa.

Hicho ndîo kipindi ambacho endapo utani-attach na Watu ili wakupe msaada ndîo wakati àmbao utakuwa umewapa ruhusa wamchukue Mkeo au Mumeo. Mahusiano mengi yalidondoka nyakati Watu wakiwa down sababu kûbwa ilikuwa Kwa Watu Husika kuomba msaada na kujiweka Karibu na Watu kupata msaada.

Taikon Master nakushauri, nyakati hizi ni Wakati wa kutulia, kuwapekeeako, kumwomba Mungu.

4. Usijilaumu wala kumlaumu Mtu. Kuwa na shukrani
Shukuru hata ukiwa down. Shukrani huifanya Akili ipate njia ya kutokea. Lawama Kwa Wengine au kujilaumu huipofusha Akili na itakufanya ushindwe Kutoka. Wengi walioshindwa kusimama ni wale waliokuwa na lawama.

Mfano, umetoka kuachwa na Mume au Mke. Usimlaumu Wala kujilaumu. Shukuru Kwa yôte. Jifunze kutokana na yaliyotokea. Hii itakusaidia kupata Mtu Mwingine Sahihi.

5. Ni Wakati kuwajua wanaokuzunguka ni watu wa aina gàni
Hiki ndîo kipindi cha kujua yupo kwako alikuwa mtu Sahihi kwako. Hata hivyo inashauriwa kwèñye VITA AU PAMBANO ni vizuri Kutengeneza anguko BANDIA ili kuwajua Adui zako Kwa urahisi zaidi na kuwafanya maadui zako wapoteze umakini wa kukushambulia.

6. Usisahau mipango yako na Wala usiibadilishe
Ukiwa down siô kipindi cha kukata TAMAA. Wengi hubadili Ndoto zào na kuyapoteza malengo Yao. Fanya tathmini, badili mikakati ila mpàngo úwe uleule.

7. Winda mawindo madogomadogo Kulingana na jinsi ulivyo-down
Usitake kulazimisha mambo Makubwa wakati unajua Kabisa upo chini. Elewa, hata Simba akiwa down huwinda Mpaka Sungura, na Wanyama wadogowadogo. Hata kama alizoea Wanyama wakubwa weñye minofu lakini akiwa down aidha Kwa kuumwa au kujeruhiwa au kutengwa na familia yake. Huwinda Wanyama wadogowadogo.

Kama ulikuwa unafanya biashara ya Milioni tano, ikatokea umefilisika. Fanya ya elfu hamsini. Hiyo NI dalili ya unyenyekevu. Haya ukiumwa utapewa maziwa au Uji au vyakula lainiaini. Lakini hawawezi kukupa Makande au Maugali. Uza Nyanya, usiwe na dharau au Kiburi.

Umesoma ndîo, lakini upo down, Acha kuchagua Kazi. Kama hutaki kuajiriwa na kulipwa Mshahara mdogo. Basi jiajiri Kwa biashara ndogondogo Zenye mitaji midogo.

8. Usiwe na haraka kuinuka
Ushaanguka, usitake kuinuka harakaharaka. Jipe Muda ujifunze Kutoka kwèñye anguko. Hoja hii inafanana na Ile ya kufurukuta. Lakini hii inalenga zaidi Mtu tayari anautulivu na hafurukuti lakini mawazo yake anajiwekea Muda mdogo wa matarajio ya kuwa down. Mfano mtu anafikiri kuwa Kwa vile Hana Ajira Basi anasema haitazidi Miaka miwili au mitatu. Hilo ni Kosa.

Kwèñye masumbwi, au ulingo wa ngumi. Ikitokea Adui anakupelekea Moto na umezidiwa, endelea kukabiliana naye ukiwa unajikinga na mashambulizi huku ukijaribu kuyazoea mashambulizi Yake na Mbinu Zake huku mara Mojamoja ukimshambulia Kwa kushtukiza.

Isome Hali. Usitake kuinuka kama hujaisome Hali ya anguko Kwa kina. Utaanguka tenà. Mara nyingi wanaopigwa TKO kwèñye masumbwi hufanya haraka kuinuka au kutaka kurudisha shambulizi ili kuwa-impress Watu matokeo Yake huishia kupikwa KO.

Mimi Acha nipumzike sasa. Nishajichokea.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
 
Mimi nachojuwa ama nime experience wazazi wanaplay big role sana kwa mtoto awe na maisha mazuri baadaye kama wao tu wako vizuri.

Watu wengi wana maisha mazuri kwasababu ya wazazi wao walikuwa vizuri.

Ni wachache sana wana maisha mazuri kutokea familia ya kimaskini kama mimi.

Angalia wote wako vizuri utakuta wazazi wao walikuwa vizuri.

Mfano humu kuna members wako vizuri kimaisha kwasababu wamekulia kwenye maisha mazuri ikawa passed on smooth and easy transition mfano Smart911 RRONDO mshamba_hachekwi min -me Kiranga Nyani Ngabu etc
 
Yeah NI kwèli Kabisa Kwa sehemu kûbwa.

Ndio Ile tunasema Maji hufuata mkondo au Mtoto wa Nyoka NI Nyoka

Exceptional ni wachache Sana
 
Mimi nachojuwa ama nime experience wazazi wanaplay big role sana kwa mtoto awe na maisha mazuri baadaye kama wao tu wako vizuri.

Watu wengi wana maisha mazuri kwasababu ya wazazi wao walikuwa vizuri.

Ni wachache sana wana maisha mazuri kutokea familia ya kimaskini kama mimi.

Angalia wote wako vizuri utakuta wazazi wao walikuwa vizuri.

Mfano humu kuna members wako vizuri kimaisha kwasababu wamekulia kwenye maisha mazuri ikawa passed on smooth and easy transition mfano Smart911 RRONDO mshamba_hachekwi min -me Kiranga Nyani Ngabu etc
Hahaha nitoe hapo mkuu🤣🤣🤣
 
Hakika, nawapa big up sana baba na mama yangu...

Cc: Mahondaw
 
Back
Top Bottom