Great deception (Project blue beam & cern)

little hulk

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2014
Posts
1,610
Reaction score
557
Habarini wana Intelijenisia...

Katika thread hii nitajaribu kufupisha maana ina mambo mengi sana. Tutajuzana zaidi pindi tutapojadili kwa pamoja. Moja kwa moja nataka nilete hii mada tupate kujuzana zaidi kuhusu dunia hii ya sasa wapi inakwenda. Kuna wingi wa conspiracy theories ambazo zilikuja kuwa ni za ukweli kama Project MKUltra : CIA Mind Control Program na Elite want to reduce the global population, so sio kila kitu ni cha kuacha kukifatilia once kikiwa na mitazamo tofauti. Katika hili naloleta laweza likaja kuwa kweli au la hivyo tuanze kulizungumzia.


Kabla sijaanza na project blue beam, nirudi nyuma kwenye miaka ya 1970 ambapo kuna maelezo ambayo yana link project blue beam na cern.

Kuna ushahidi wa Dr. Carol Rosin alioutoa miaka ya 2000 kipind yeye akiwa anafanya kaz kama "space and defense consultant" katika mwaka 1974 mpaka 1977. Alifanya kazi na Wernher Von Braun ambae ndie aliyempa maelezo abayo yeye (Dr. Rosin) alikuja kuyatoa baadae kama ushahid wake kwa vitu vinavofanyika nyuma ya pazia.

Braun alikuwa mwanasayansi mjerumani aliyekuwa anafanya kazi marekani ambapo alikuwa nafanya kazi inayohusiana na uwazishwaji wa "space - based weapons". Katika kipind chake cha kuumwa cancer alipata kuongea na Dr. Rosin kuhusu strategies inayofanywa na elite kupitia serikali kubwa dunian kufanikisha uwazishwaji wa "space - based weapons". kufanikisha hivyo ilitengenezwa mkakati wa kuweka au kujenga hofu duniani, "scare tactics" ambazo zitafatwa ili yatimie malengo yao. Dhumuni la mkakati huo ni jinsi ya kumtambua adui na hatua gani zifatwe ili kumdhibiti adui huyo (adui ni mleta hofu/woga katika jamii za watu) Hivyo maadui waliotengenezwa au hatua ambazo zitafatwa kufanikisha jambo lao ni:
· Cold war
· Terrorism
· Countries of concern (third world countries)
· Asteroids, na
· Alien Invasion
Itaanza vita baridi kati ya USA na Russia, itafata Ugaidi ambao tunauona mpaka sasa, itafata africa (hapa sijafahamu tuta contribute vipi katika plan yao ya uwazishwaji wa "Space - based weapons"), itafata mawe au vimondo kushuka duniani (source: Asteroid size of Statue of Liberty to hit Earth | World | News | Daily Express)na mwisho ni alien invasion. Ambapo haya yote unayasikia. Shida ni kwamba hiyo "Space - based weapons" sio dhidi ya mawe yanayokuja kutoka outer space ili tuyalipue kabla hayakajika duniani, au kuzua invasion yoyote ya extraterrestrial beings wowote ambao wata onyesha ku threat dunia, ila hiyo project ni dhidi ya watu wa dunia hii ili ku-control population. Hii itapelekea katika uwazishwaji wa New World Order
[Dr. Rosin anaamini kuwa aliens wapo na walishakuja ku visit earth lakini hawajawahi ku-threat the earth peace, pia kuna maelezo ambayo alitoa Rais wa marekani Ronald Reagan alizungumzia kuhusu watu wa kabila zote tupate kuwa pamoja tuache tofauti zatu dhidi ya alien threat kama ikitokea]
source:
· https://socioecohistory.wordpress.c...st-card-will-be-the-extra-terrestrial-threat/
· https://www.youtube.com/watch?v=iQxzWpy7PKg

Sasa katika kufanikisha kuleta NWO Project Blue Beam na CERN zitahusika. Ukianzia katika ushahid wa Dr. Rosin unakuta baadhi ya maadui washagundulika na washafanyiwa na wanafanyiwa kazi, kama vita baridi na Ugaidi. Ila tukizungumzia kuhusu Asteroids na Alien Invasion ni lazima technology itumike, ndipo Project Blue Beam inatumika.

Project Blue Beam
According to Wikipedia "Project Blue Beam is a conspiracy theory that claims that NASA is attempting a New Age religion with the Antichrist at its head and start a New World Order, via a technologically-simulated second coming."

Ni top secret operation ya NASA kufanikisha kuleta ONE World religion. kama wikipedia inavosema na vyanzo vyengine inaaminika kwamba NASA wana plan wa Kuleta Ujio wa wa pili wa Messiah, ili kufanikisha hivyo lazima watatumia hologram display katika anga na ku onyesha ujio wa Messiah. Hii itawezekana maana kuwatumia vifaa vyao vyenye technology ya juu pia zilizopo nje ya anga na ndani ya anga kuonyesha ujio wa Messiah.

Anga ya sasa ni tayari a LCD screen maana tayari washaweka na wanaendelea kuweka compounds ambazo zinapatikana katika chemitrails zinazotolewa na ndege (airplanes). Pia kupitia HAARP (High Frequency Active Auroral Research Program) ambayo ni "weather weapon" inauwezo wa ku twist hali ya hewa. [hii nitaielezea kwa threads za mbeleni, ni ndefu kidogo]. Hivyo Project Blue Beam plus HAARP hii event ya ujio wa messiah itaonekana real event.

Kwa sasa Project Blue Beam tests zake ni za UFO sightings ambazo zinazidi kuongezeka. Hologram display technology imefanika sehemu nyingi kama majaribio au for entertainment kama



· hologram display ya Prince Charles wa uingereza alivotokea katika mkutano uliofanyika Abhu Dhabi
· 2pac aki perform live concert katika coachella music festival in 2012 ( https://www.youtube.com/watch?v=TGbrFmPBV0Y )
· Kipindi Rais Obama anapewa tuzo ya Noble Prize nchini Norway mwaka 2009, spiral ilitokea angani usiku huo na kutengeneza black hole
· Mwanga wenye umbo la Bikra Maria (kama tulivoseshwa kumuona katika picha na statue) alioneka Ivory Coast April 2011 ( https://www.youtube.com/watch?v=IvyUnmBjxm8 )
kwa kufahamu zaidi kuhusu step nne watakazo fanya ili kufanikisha agenda yao please pitia hapa: Project Blue Beam | NEW WORLD ORDER PLAN

Hivyo katka kutimiza YOTE hayo ndipo unakutana na CERN ambayo ina marefu yake kuielezea.


CERN
Kiufupi CERN ni Conseil Européen pour la Recherche Nucléaire au European Organization for Nuclear Research. CERN inahusika na particle physics experiments ambapo ndo the largest machine in the world ambayo imejengwa underground kwa mzunguko wa 4700 miles imejengwa uswisi na kupitia katika mpaka wa ufaransa na uswisi.

CERN wamejenga Large Hadron Collider (LHC) kwa dhumuni la ku discover "GOD'S PARTICLES" au "Higg Boson". Kwa lugha nyepesi wanataka kujua particle inayo hold everything together (like atom ina neutron, electron na proton ambazo nazo zina subatomic zake kila moja, hivyo wanataka kujua the tiniest or smallest particle that is invisible but do exist, ambayo ndo higg boson experiment)
Kuielewa zaid CERN, yenyewe ndo ya kwanza kuanzisha world wide web "www", wao ilikuwa kwa ajili ya ma researchers kuwasiliana na bbade wakaitoa kwa public.
Turudi katika mada yetu, CERN wanafanya experiment za kugonganisha proton kwa proton ili kupata other particles katika detectors zao.

Wao CERN wanadai kwamba wakifanikiwa kupata God particles wataweza ku discover the door or a gateway ambayo wataweza ku discover vitu kutoka huko au kutuma kitu kwenda huko.

WHAT IS A GATEWAY OR A DOOR THAT CERN EXPECT TO DISCOVER?
Nikikurudisha nyuma kidogo kuhusu CERN, kuna kitu kinaitwa ANTIMATTER ambayo CERN imetengeneza LHC ili iweze ku discover ku hold na ku control anti matter. Inasemekana kuwa antimatter is very unstable so inaweza ikaleta destruction duniani. Hivyo kupitia antimatter wataeza kupata God's particle.
Hili ndo linalowaogopesha wengi kwa wanaofatilia kila wanachokifanya CERN, kwamba they want to create a portal au vortex ambayo ita link parallel universes.
Parallel universe kama inavotamkika ni universes ambazo hazikutani kabisa. Mfano sisi Binadamu ni certain dimension (to be exact 3rd Dimension beings) hivyo kuna Dimensions zingine ambazo hatuwez ku interact nazo. So mlango (a gateway) utakaopatika CERN utakuwa umeanzisha inter-dimension between different universes.

WHY IT BECAME A CONSPIRACY THEORY?
Kwanza kabisa CERN wameuita mwaka 2015 kuwa "INTERNATIONAL YEAR OF LIGHT". Kwamba lile swali tulilokuwa tunajiuliza kuhusu BIG BANG THEORY liko karibu kujibiwa maana pindi LHC ikiwashwa kwa energy kubwa ambayo ni 13 TERA ELECTRO VOLTAGE (13TeV) ambayo haijawahi kufanya kazi kwa nguvu hiyo ambapo itakuwa na uwezo wa kuzungusha proton kwa speed nearly speed ya mwaga (speed of light) ili kufanikisha collision kubwa haijawai tokea ili wapate God's particles ndipo watajua kuwa origin ya universe ni nini.

Pili kuna sanamu la Mungu wa Kihindi (SHIVA) katika Headquarter yake. Ukifatilia SANA kuhusu God Shiva ni Mungu wa kihindi mwenye maana ya "The Distroyer". Swali ni kwanini wameamua kumweka Shiva, Hivyo imebaki kuwa na majibu mengi ila majibu machache ni kwamba endapo watakapoweza kufungua huo mlango " a gateway" Shiva ambaye ndo the Distoryer ambaye pia anaaminika kuwa ndo Lucifer atatoka. Jibu lingine kwamba watatoka spritual beings ambazo ni demons ambapo watakufa watu wengi sana maana the only energy ya ku fungua mlango huo people's souls, jibu jengine ni kutoka kwa Antichrist ambaye atafanya wonders na watu kumfata, na la mwisho ni kukutana kwa mara ya kwanza na extraterrestrial beings.

MAWAZO MENGINE
Nikiingia katika iman ya kikristo yenye maelezo ambayo yanaweza kuipa mada hii changamoto ni Mnara wa babeli. Wengi tunajua habari ya mnara wa babeli ambao watu wa kale walijenga mnara ili kilele chake kifike mbinguni ili wasipate kutawanyika uson mwa dunia na wajiapatie jina kupitia hapo.
Mwanzo 11:1 Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja.
2 Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko.
3 Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa.
4 Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote.
5 Bwana akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu.
6 Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya.
7 Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao.
8 Basi Bwana akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji.

Kwanza tupate kujua kuwa nia yao ilikuwa kufika Mbinguni na Bwana akasema hawa hawatazuiliwa kwa neno lolote ikimaanisha hawashindwi kitu kwa watakachoamua kukifanya hivyo akawabadili lugha.

Sasa waliwezaje kutaka kufanya mnara ufike Mbinguni wakati Mbinguni ni other than spiritual world? Na ukiangalia kwa sasa hivi ni ngumu kujenga mnara ambao utakaoweza fika mawinguni, sasa hao waliwezaje kutaka kujenga mnara ufike Mbinguni!!??

Well kwa mtazamo mwengine walikuwa wanajenga mlango wa kwenda mbiguni (walikuwa wanajenga kitu ambacho kina link different dimensions "a gateway" ) kama wanavyofanya CERN kwa sasa.
Hivyo Hii ya CERN ikifanikiwa na atakayetoka katika huo mlango ndo atakuwa the new Messiah ambaye ni Antichrist ambaye pia ni Nephilim (other claims that) - Nephilim ni offspring kati ya mwanadamu na fallen angels [DNA crossover].

I, PET GOAT II
Hii ni video ambayo inahusiana na mambo yote ya kuleta new messiah pamoja na New religion na NWO. check youtube
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…