Wewe kama great thinker, naomba leo tujadili swala la vyanzo vya mapato ambavyo serikali yetu aidha imevisahau au haijui kama vinaweza kuza Pato la Taifa, naomba uorodheshe vyanzo vya mapato (kodi) ili tuisaidie Tanzania.
1. TRA ipanue matawi yao hadi maeneo ya vijijini ili kutoza kodi kwa wafanyabiashara wa maduka na biashara zingine ambao hata leseni ya biashara wengi hawana.
2. Kwenye kingo za mito na maziwa huko vijijini ambapo wavuvi wengi hupata pesa wauzapo samaki lakini hata ushuru wa kawaida hawalipi.
3. Kwa wachimba madini wadogo waliopo vijijini ambao wanapata pesa lakini kodi hawalipi.
4. Kuwepo na kodi ya Bima kwa mwaka mara moja kwa chochote ulichowekea bima.
5. Kuwepo na extra tax ambayo itakuwa ya hiari kulipwa na wafanyabiashara wa kati na wakubwa kwa mwaka mara moja ila kwa mfululizo miaka 3 kwa kiasi kisichopungua million 150 za kitanzania kwa kila mfanyabiashara au kampuni halafu wanapewa tax holiday ya mwaka mmoja na nusu tu pia na mfanyakazi mmoja wa hiyo kampuni kupewa na serikali exposure ya kwenda abroad kwa mafunzo ya transfer of technology juu ya taaluma yake kwa miezi 8, Kisha arudi Tanzania na kupewa assignment ya kufundisha taaluma hyo kwa vijana kwa kuanzisha community small industries huku akiendelea na ajira yake.