Mkuu mawazo yako yako powa sana but kwa mambo jinsi yanavyo enda ni vigumu sana.
1. Kuhusu rural Industrazation
- Kwanza watanzania wengi hawapendi kuanzisha viwanda vidogo vodogo, wana penda sana biashara zi sizo umiza kichwa
- Sera ya sasa ni mbaya sana, na tusipo angali swala la viwanda Tanzania halitakuwepo tena, serikali isipo dhibiti importation ya kila kitu kutoka china, itakuwa vigumu sana ku shindana
2. SACOSS
- SACOSS zilikuwa zamani, kwa sasa sakozi zimekamatwa na mabenk na zimegeuzwa kuwa mawakala wa mabenki, zinatoa mikopo yenye riba sawa na benki
- SACOOS nzuri ni ambayo itajitegemea yenyewe kifedha yaani sikope benk
3. Hivi vikundi vya wilaya siasa zimekuwa nyingi sana
4. Mkuu swala la mikopo inatakiwa uanze na fund yako kwanza, tafuta fund yako hata kama ni kidogo anza nayo na soma on how to manage business money itakusaidia sana kukua
Nimekupata vizuri mno Komando na ninakubaliana nawe kwa sehemu Fulani but nina mambo kidogo ya kushare na wewe. Nitafuata namba kama ulivyofanya, but kwa ruhusa yako naomba kusema kwamba hizo ni wishes tu
1. Hapa umegusa kwenyewe kwani nami nikiangalia naona watoa huduma na si actual producers (
hii ni mbaya sana Kiuchumi). Sasa issue ni kwamba tutabadilisha vipi hii trend?
2. Mimi nipo SACCOS na ni kiongozi, hivyo najua zinavyoendeshwa na maamuzi yanavyofanyika hivyo nikakubali nyingi zimegeuka kama mawakala wa Benki. Vile vile ukiangalia masharti ya mikopo ya baadhi ya SACCOS na interest zao (2% per month) tena flat rate ni afadhali uende Bank kama NMB (
nimefanyia research hii kitu). But ni ujinga wa wanachama ndio unasababisha haya, kwa namna trend ilivyo sasa hivi mnaweza mkaitumia kwa faida yenu kama kikundi (SACCOS). Hizi Saccos zinakopeshwa na let say na CRDB Microfinance Plc kwa 9& p.a inakuwa vipi wao wakopeshe kwa 24% wanachama ambao ni wamiliki. (hapa kuna ongezeko la 15%). Sasa utagundua Saccos nyingi zimekodisha maeneo yenayolipiwa kodi kubwa, wameajiri watumishi wengi wanaolipwa pesa nyingi na defaulf rate ya wakopaji (
wanachama) ipo juu (
this has nothing to do with the banking strategies na huu ni mzigo unaopelekwa kwa wanachama kwa njia ya riba). But we can change this. How? Hii ni maada nyingine.
3. Ni kweli siasa kwenye hivi vikundi zinazidi kuwa nyingi. But tatizo ambalo ninaliona ni vikundi vingi kukosa wasomi na vijana ambao ni visionaries, hivyo vinaingiliwa na wanasiasa kwa maslahi yao. Ndio maana natamani wajasiriamali vijana na wasomi waingie huko. Mimi ni mmoja wa wanachama wa TCCIA na ninasubiria majibu ya application yangu CTI.
4. Hapa ninashukuru kwa ushauri, ila naomba nikupe report kuwa fund kidogo pamoja na vitendea kazi kama MIS, computers, usafiri wa offisini, copier, fax/telephone na office furnishings tayari vipo in place na leo nimetoka kupeleka memarts BRELA kwani ninasajili kama Company Limited by Guarantee then ndio natafuta Certificate of Compliance kwa Registrar wa NGO. Research ya products zinazotakiwa sokoni imefanyika kwa muda wa mwaka Mzima na nimeende shule (
http://www.samtraining.org) kwa ajili ya kupull off hii kitu
Thanks.