Manchester United imetangaza kwamba Mason Greenwood amesaini kandarasi mpya ambayo itamuweka klabuni hadi Juni 2025.
Greenwood ni zao la Academy ya klabu na amekuwa huko Manchester United tangu umri wa miaka saba.
Mchezaji huyo wa miaka 19, ambaye ni mfungaji mdogo zaidi wa United aliyewahi kufunga magoli kwenye mashindano ya Uropa, tayari ameshacheza mechi 82 klabuni hapo.
"Unapojiunga na klabu katika umri wa miaka saba, unakuwa na ndoto ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza siku moja". Alisema Greenwood
"Mason ni talanta nzuri na bado ni mfano mzuri wa aina ya mchezaji ambaye Academy yetu inazalisha". Alisema Ole Gunner Solskjaer