Thomas Lazaro
Member
- Jul 28, 2020
- 5
- 1
UTANGULIZI
Kutokana na kukua kwa tatizo kubwa la ajira miongoni mwa vijana na familia nyingi duniani, imepelekea watu kuchanganyikiwa ni nini cha kufanya. Watu wote siku hizi wanahaha kutafuta ajira ambayo imekua adimu sana na hivyo kuwafanya watu ambao akili zao na mawazo yao yameelekezwa kwenye kuajiriwa kupata msongo wa mawazo na hata kupata matatizo ya kiafya inayosababishwa na stress
Miongoni mwa waathirika wakubwa wa tatizo hili la ajira ni pamoja na wahitimu wa shule na vyuo mbali mbali duniani. Tatizo la ajira ni janga la kimataifa katika kizazi cha sasa kwani wanafunzi mashuleni na vyuoni wameandaliwa kuwa waajiriwa badala ya kuwa watengeneza ajira
Kitabu hiki kimelenga kuwafungua watu kutoka kwenye kifungo cha ajira kama njia pekee ya kupata kipato na inafundisha mbinu na njia nyingine ya kupata kipato ya kuanzisha biashara na uwekezaji
Pia kitabu hiki kimelenga kuwaandaa matajiri wakubwa ambao watakuwa waandaa ajira kwa watu wengine. Niamini baada ya kukisoma kitabu hiki na kuweka ulichojifunza kwenye matendo hakika utaishi kujua njia nyingine mpya ambayo ndio chanzo kikubwa cha utajiri na utakuwa suluhisho la ajira kwa wengine pia.
Elimu na ufahamu utakao upata kwenye kitabu hiki utakufanya ugundue kuwa utajiri unao wewe mwenyewe kwenye mikono yako na wala hauitaji kuwa na mtaji mkubwa sana kuanza biashara na uwekezaji utakao kufanya kuwa tajiri. Vile vile kwa wale ambao wameajiriwa watajikuta wanaanza kupata njia sahihi ya kuwa tajiri badala ya kutegemea njia moja ya ajira kuwa chanzo pekee cha kupata kipato.
Waajiriwa watagundua pia kuwa ajira ni sehemu ya kujifunzia kufanya kazi za uwekezaji na biashara. Badala ya kugombana na mabosi wao kila mara kuhusu kuongezewa mishara, kutegemea promotion za kazini, kufanya ufisadi na rushwa kama njia ya kujiongezea kipato, watajifunza kujiongezea mishahara na kujipa promotion wao wenyewe kupitia biashara na uwekezaji wao wenyewe.
Miongoni mwa chanzo cha kupotea kwa ajira nyingi duniani ni pamoja na kukua kwa sayansi na teknolojia ambayo kwa upande mwingine ungeweza kutumika kuwa jukwaa zuri la kutatua tatizo la ajira. Ebu jiulize; je unajua fursa zinazopatikana kutokana na uwepo wa sayansi na teknolojia ikiwa ni pamoja na ukuaji wa mitandao ya kijamii?
Je, huwa unaitumiaje mitandao ya kijamii, kwa kuchati au, kwa kutangaza biashara yako?
Mitandaoni kuna fursa nyingi ambazo hazijawahi kuwapo na ni fursa kwa watu wote bila upendeleo wala ubaguzi wa kipato hata kama hauna kipato kabisa unaweza kuanza biashara kupitia mtandao na ukawa tajiri. Ebu endelea kujifunza kupitia kitabu hiki.
