The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 747
- 2,112
Rapa Gsan wa kundi la X Plastaz kutoka Arusha
BET Cypher, kama inavyojulikana na wengi, ni sehemu ya BET Hip Hop Awards ambayo husubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa Hip Hop duniani kwani huwahusisha miamba wa muziki huo kutoka maeneo mbalimbali duniani. Gsan alishiriki akiwa pamoja na magwiji kama Eminem na KRS One, lakini pia Nipsey Hussle, aliyekuwa akiibukia katika ulingo wa Hip Hop wakati huo.
Gsan (katikati) akiwa na KRS One (kulia) pamoja na DJ Premier (kushoto)
Na hivyo ndivyo Gsan alipata fursa ya kukwea pipa kuelekea Brooklyn, New York kurekodi cypher na baadaye kuhudhuria kilele cha tuzo hizo Jijini Atlanta, Georgia.
Ingawa Hip Hop kwa Kiswahili lilikuwa suala geni, lakini magwiji wa muziki huo kutoka Marekani, KRS One aka Teacha pamoja na DJ Premier walikoshwa sana na vionjo hivyo vya Kiafrika. Gsan hakufanya ajizi kuipeperusha bendera ya Tanzania.
Tazama video hii kumuona Gsan akiwakilisha Tanzania miongoni mwa magwiji wa Hip Hop duniani
“Kwangu ilikuwa kitu kikubwa sana kuwepo sehemu moja na watu kama Eminem, KRS One, huku DJ Premier akipiga midundo na mimi nikionesha kile nilicho nacho. Wengi walifurahishwa na nilichofanya na kuniuliza kwanini nili-rap kwa Kiswahili kwani walitaka kuelewa nichowasilisha. Niliwaambia Kiingereza si lugha yangu ya kwanza ingawa naizungumza na ninapenda”, alisema Gsan katika mahojiano baada ya uwakilishi huo.
“Kulikuwa na emcees kutoka duniani kote kwenye eneo moja na nilifurahi kuiwakilisha Afrika. Sikupigwa na butwaa kuwepo pale na wasanii wakubwa duniani, bali nilifurahi kuonesha uwezo wangu mbele ya marapa wenzangu.”Gsan akiwa na rapa Nicki Minaj wakati wa BET Hip Hop Music Awards mwaka 2009 Atlanta, Georgia. Kabla ya hapa Nicki na Gsan walikuwa tayari wameshakutana katika Cypher Brooklyn, New York.