GSM acheni kuwatumia Wasemaji na Wazee wa Yanga SC Kuwachafua Waziri Mkuu Majaliwa na Rais wa TFF Karia kwa Maslahi yenu ya Kibiashara

GSM acheni kuwatumia Wasemaji na Wazee wa Yanga SC Kuwachafua Waziri Mkuu Majaliwa na Rais wa TFF Karia kwa Maslahi yenu ya Kibiashara

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Nimependa nilipoona TFF imetoa ONYO juu ya Upuuzi huu wa Wasemaji na Wazee wa Yanga SC ila nashangaa na nasikitika mpaka leo Wizara husika ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na BMT wakiwa Kimya kitu ambacho ni Hatari na kinaweza kuibua Hisia Mbaya juu yao.

Baada ya GSM kuona Mkakati wao Kufeli kwani baada ya Tangazo lao la Kujitoa kama Wadhamini Wenza wa NBC Premier League GSM walitaka Umma ( Public ) ukasirike, presha iwe Kubwa, Waogopwe na Wamharibie Rais Karia wa TFF na Watendaji wote wa TFF.

Aliye nyuma ya huu Upuuzi na Uhuni wote uliofanywa na unaendelea Kufanywa na Wasemaji wa Yanga SC na jana Wazee wa Yanga SC na nimeambiwa kuna Kundi lingine litaibuka kabla ya Jumapili au kutatokea Tukio fulani ili tu Mkakati huu Maalum wa Kuichafua TFF na Serikali ( hasa Waziri Mkuu Majaliwa ) ambao Wote hawa ni wana Simba SC Kiushabiki / Kimapenzi utimie.

Na sisi Wadau wa Michezo tunawasubiri hawa Wazee wakienda huko wanakotaka kwenda Kushtaki wamtaje Waziri Mkuu Majaliwa ili na Sisi tuwakumbushie hawa Wazee jjnsi gani Rais Mstaafu Kikwete nae aliwabeba Yanga SC tena wazi wazi na muda mwingine Kumtumia Mwanae Kipenzi Ridhiwani Kuihujumu Simba SC na kuweka Msukumo kwa TFF iliyokuwa chini ya mwana Yanga SC Mwenzao Jamal Malinzi ili Washinde na wawe Mabingwa mfululizo kwa Kipindi kile.

Mnashindwa Kucheza Mpira na mnaanza Kuwachafua Viongozi Waandamizi wa Serikali kuwa Wanawaonea mkidhani Watanzania wote ni Wapumbavu ( Fools ) kama mlivyo na Klabu yenu mkisahau kuwa Kuimba ni Kupokezana hivyo na sasa Simba SC wameshajjtathmini, wamejisahihisha na wanaanza kurejea katika rythm yao ambayo mara nyingi huwa inawafanikisha kuwa Mabingwa.
 
Simba, Yanga na TFF ndio Cancer ya soka la bongo.

Huwezi kuwa kiongozi Simba, Yanga na TFF kama wewe sio mtoto wa mjini na mission town, wote waliowahi kuwa viongozi Simba, Yanga na TFF lazima wawe wapigaji wa mjini, Samora, Salamander, Clock tower, Kariakoo..nk Kama wewe sio mission town wa hayo maeneo huwezi kuwa kiongozi Simba, Yanga na TFF..

CCM na Serikali iache pia kuvitumia vyombo hivi kisiasa baadala yake vibaki huru kwenye majukumu yao kwa maslahi ya soka la Tanzania.

Soka ni ajira kubwa sana duniani, Siasa ikiacha kutumika kwenye soka, Vijana wetu wengi sana watapata ajira kupitia tasnia ya mpira na Taifa litaingiza kipato kikubwa sana na hata Timu yetu ya Taifa itafanya vizuri...
 
Ndugu hongera sana kwa haya Madini yako mazuri, ya kweli na ambayo kiukweli nimeyapenda mno.
 
[https://res]

MWENYEKITI wa Bodi ya Ligi Kuu Bara, Steven Mnguto, ameibuka na kusema licha ya wadhamini wenza Kampuni ya GSM kutangaza kujiondoa katika udhamini lakini hakuna klabu yoyote iliyolipwa.

Kauli hiyo imekuja ikiwa ni siku moja tangu GSM watangaze kujiondoa kudhamini klabu za ligi ambazo awali waliingia mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Sh 2.1Bil.

Akizungumza na Championi Jumatano, Mnguto alisema kuwa, hilo suala wamepanga kulizungumza hivi karibuni
mara baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) watakapokutana.

Mnguto alisema kuwa, wanasubiria wanasheria wao walipitie suala hilo na mwisho wa siku watalitolea ufafanuzi
kwa undani.

“Kiukweli tangu tuliposaini mkataba na GSM nikiri klabu hazijapata chochote. Klabu zimeitangaza GSM kwa muda wa miezi mitatu sasa, kwa hiyo tunasubiri wanasheria walipitie suala hilo tujue tunafanyaje.

“Hata suala la zile nembo kwenye mabega sijui kama zinaweza kutolewa haraka lakini hata hilo litafanyiwa
kazi kisheria,” alisema Mnguto.

Naye Mkurugenzi wa Habari na Masoko wa TFF, Boniface Wambura, akizungumzia hilo alisema: “Sisi
baada ya kupata barua kutoka GSM, suala la mkataba ni Bodi ya Ligi na ni vema akatafutwa Mnguto lakini
kwa upande wa sisi TFF hatuwezi kuzungumzia kila jambo.

“Tayari tumetoa tamko letu jana (juzi) kuhusiana na hilo baada ya kupata barua GSM.” Juzi TFF ilitoa taarifa
kuwa, Februari 7, mwaka huu walipokea barua ya kuvunja mkataba wa udhamini mwenza wa Ligi Kuu Bara
ya NBC kutoka Kampuni ya GSM, hivyo Shirikisho hilo linafanyia kazi barua hiyo na litatoa taarifa kwa wadau.
 
Back
Top Bottom