Kuhusu wafungwa kuna baadhi ya nchi za ulaya zimekubali kuwapoke na wahukumiwe kwa sheria za kiraia na sio za kijeshi. Na leo kwenye CNN nilimuona mmojawapo wa aliyekuwa mtuhumiwa wa Guatenamo ambaye ameachiwa huru akisema kwamba wanampango wa kuishitaki Serikali ya Merikani ili imlipe fidia kwa madhila aliyotendewa pamoja na maumivu aliyoyapata.
Nadhani kwa wate wote ambao hawataonekana kwamba hawana hatia wataruhusiwa kurudi katika maisha ya kawaida ili swala linaloendelea kuwaumiza vichwa ni wapi watarudishwe. Kwa sababu hofu yao ni kwamba wakirudi nchi zao za asili yawezekana kabisa wasitendewe haki au wakaanzisha mapambano dhidi ya marekani kwa madhila waliyotendewa pindi walipofungiwa kwenye hili gereza.
Kule Iraq alidai ndani ya miezi 16 anategemea atakuwa ameshawaondoa wanajeshi wake wote na kuwaachi wenyewe wajitawale. Ila cha kushangaza ni kwamba hao hao wanajeshi anafikiria kuwapeleka Afiganistani ili kuleta amani.
Labda Mrs Clinton atatuhabarisha zaidi ni lini hizi sera zao watazikamilisha. Manake yeye ndio amekamata cheo cha Secretary of State na jana aliapishwa rasmi na leo ameanza kazi.
Du kweli inashangaza mimi nilifikiri hata hawo wajeshi wa afghanistan anawarudisha nyumbani.
Mimi wakati mwingine huwa nafikiri hata huyo Osama wanayemsema ame tengenezwa tu hata hayo majengo ni bush mwenyewe ndiye aliyabomowa ili apate sababu za kumnyonga SADDAM ,akianzia kupitia Afghan na kupata sababu ya kuelekea kwa mlengwa wake.
Sasa kwanini basi Afghan iendelee kukaliwa na walowezi?