Gubu la mawifi

Gubu la mawifi

Anita Baby

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2011
Posts
1,265
Reaction score
540
Nina wifi angu ambaye ndo wa mwisho kwao mume wangu. Amekuja baada ya kuhitim form four. 1st time nilimuona ni binti mpole sana but baada ya wiki mambo yakabadilika. Ananuna hovyo hata cjui sababu nin? Unaweza ukamuuliza kitu akajibu tu kwa ishara bila kutamka lolote. Kuna majirani nili mtahadharisha asiowazoee kwa sababu ya tabia zao za umbea na uongo walio nao. Cha kushangaza ndo kawa rafiki zake. Nifanyeje?
 
Hilo sio gubu la wifi ni gubu la teenager.
Watoto bwana, ukiwaambie usichezee maji ndio anachezea. Hukua na haja ya kumkataza kuwa rafiki nao kabla hajaonyesha kutaka kufanya hivyo.

Jaribu kua unaongea nae taratibu badala ya kugombeza,kuagiza na kuonyesha kwamba
unampangia maisha.
 
jamani katoto ka miaka 17 nako mnakaita wifi na kukapa respect ya uwifi? Acheni hizo bana,just treat her like a kid,command her na umpe maelekezo na akutii.
 
teenager huyo,atakuwa anaona wivu unatoka na kakake
 
Sijawahi kuishi na wifi (sina) ila nimeona kwa mdogo wangu, yuko very authoritative; na mawifi zake wote wanamtii. Kweli mtoto wa form four nae anataka apigiwe magoti. Ni kumwambia tu marufuku kufanya one two three; finito.

jamani katoto ka miaka 17 nako mnakaita wifi na kukapa respect ya uwifi? Acheni hizo bana,just treat her like a kid,command her na umpe maelekezo na akutii.
 
asikuumize kichwa anakaa kwako afate principals za humo ndani nothing less
 
mama ndo kiongozi wa nyumba, sasa inakuwaje hako katoto kakuchezee?? pitisha sheria zako na kama hataki kufuata arudi kwa wazazi wake, umeolewa na mmoja na sio mia moja.
 
Kwani ilikuaje akaja kukaa kwako? Ndo kahamia au kaja kwa matembezi? Km kaja kuishi na ww inabidi akutii na afuate principles zako. Kwanza mtt mwenyewe ndo kwanza kamaliza f4, at least angekua na kazi yake ya kuweza kumkim matumizi yake. Kama haelewi somo mwambie kakaake na akiwa anakukosesha raha arudi kwao tuuu
 
Kwanza we una umri gani? Nina maana je umepishana na wifi yako kwa miaka mingapi? lakini km wengi walivyosema ni yuko ktk foolish age, muelekeze kama mdogo wako, mkaripie anapostahili mpangie kazi za kufanya, muelekeze kama mama na mwanae.

Pole sana ila mchukulie kama mdogo wako ambavyo ungemchukulia (inategemea na mlivyopishana)
 
lakini nyie sometimez mawifi hawa mmhh tunaweza sema ni mtoto lakini huwezi jua source hasa huwa pengine kimeskia dada zake wanakuongea vibaya au hata mama ,pengine unajaribu tuu kutoa ushauri ambao hata mdogo wako wa damu ungefanya the same ila ikija kwa wandugu wa mume inakuwa kero wanaona kama unawaingilia ..inahitaji hekima kuishi na mawifi no matter ni mdogo kiasi gani..mm najiwekaga kando ya nn nijipe stress za bure 4 wat?
 
Nina wifi angu ambaye ndo wa mwisho kwao mume wangu. Amekuja baada ya kuhitim form four. 1st time nilimuona ni binti mpole sana but baada ya wiki mambo yakabadilika. Ananuna hovyo hata cjui sababu nin? Unaweza ukamuuliza kitu akajibu tu kwa ishara bila kutamka lolote. Kuna majirani nili mtahadharisha asiowazoee kwa sababu ya tabia zao za umbea na uongo walio nao. Cha kushangaza ndo kawa rafiki zake. Nifanyeje?

Wewe umelitaka mwenyewe. Kumwambia kuwa watu fulani ni wambea asizoeane nao ndo umeharibu kwani hiyo ni ishara mabaya ya kutaka kuficha mambo yako. Ndo maana umehamaki kuona kuwa amekuwa rafiki na wale ambao wewe unawaogopa. Cha msingi jipe moyo utashinda
 
Back
Top Bottom