Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Beki wa kati wa Crystal Palace na England, Marc Guéhi huenda akachukuliwa hatua za kinidhamu na Shirikisho la Soka la Uingereza (FA) baada ya kuandika “I LOVE JESUS” kwenye kitambaa chake cha unahodha wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Newcastle mchezo uliomalizika kwa sare ya 1-1 jumamosi ya Novemba 30.
Vitambaa vya unahodha vyenye rangi ya upinde viligawiwa kwa vilabu vyote 20 vya Ligi Kuu kwaajili ya kusaidia jumuiya ya LGBTQ+, hivyo uamuzi wa Guéhi wa kuongeza ujumbe wake binafsi unaohusu dini unaweza kuchukuliwa kuwa ni ukiukaji wa Sheria za Mchezo kwani vitambaa hivyo haviruhisiwi kuandikwa kitu chochote cha kibinafsi.
Soma, Pia: Nahodha wa Ipswich Town, Sam Morsy agomea kuvaa kitambaa cha Unahodha chenye Upinde kwa sababu za Kidini
Soma, Pia: Nahodha wa Ipswich Town, Sam Morsy agomea kuvaa kitambaa cha Unahodha chenye Upinde kwa sababu za Kidini