Guest gani bei ya chini zanzibar?

Hii ni nzuri sana na ni ya kawaida inaanzia Tsh 35,000 tatizo ipo karibu na ukumbi wa CCM Maisara hapo kunakuwa na dansi na kelele nyingi ,pia inabidi uwe na hela ya taxi kwenda mjini hakuna daladala karibu ,kama unapenda mjini naona ADAMs ipo Malindi ukitoka bandarini inatazamana na klabu ya soka ya malindi hapo ni sh 35000(sio self) ukitaka selfu ni 40,000 ni karibu na town ,bandarini na hata ukitaka kutembelea bustani ya ya pale bandarini karibu na Mji Mkongwe ni poa huhitaji taxi na pia ni salama
 
za chini sana pia zipo za sh 12,000 ipo pale darajani karibu na makao makuu ya CUF nimesahau jina ukiuuliza watu wa taxi watakupeleka
 
mzuri,ipo hapo club ya malindi,kwa nje pamechoka,ila ndani burdani,ila ukiwasha Ac bei inaongezeka,ni shs 25,000 bila ac,ukingurumisha inakua 35,000 pia mizigo sijui kama inakubalika!manake wale wana sheria kali.
 
Mkuu kwa Zanzibar usalama siyo tatizo kama huku kwetu.Ila ukitaka kuenjoy kwa gharama ndogo na kuepuka inconvenience tafuta guest maeneo ya Darajan(hapa ndiyo mjini kwao)i,Stone town(aka mji mkongwe) na Malindi.Kama eneo hilo analosema mkuu bujibuji lipo ndani ya stone town.Chukwani na Airport sikushauri kwa sababu ya mambo ya kupanda taxi ama daladala which may not be convenient for a stranger na hsa kama unakaa siku moja au mbili tu.
 

Haha! Rate ya chini kabsa ni kama us 600. Nenda Mbawala pale, karibu na Amaan fresh,kama jina lilivyo huyu nadhani ni mngoni mwenzio so mboga zote utakula. Ila inabidi uende kipindi hichi wakti Al shaabab tuko bize kulipuwa kenya-otherwise moto njenje pale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…