Position ni kuwa hata hapa kwetu ni hivyo. Katiba yetu ya mwaka 1977 kama ilivyorekebishwa ina kitu kinaitwa presumption of innocence. See Article 13 ( 6 ) (b).
Tatizo liko kwenye vyombo vya upelelezi eg polisi, takukuru etc, bunge, mawakili na mahakama.
Tatizo lililopo ni jinsi gani wapelelezi wa kesi wako mahiri katika kupeleleza kesi zao. Sheria zetu zinaruhusu dhamana wakati wa upelelezi ( police Bail), hii inasaidia mshukiwa pupewa dhamana wakati upelelezi unaendelea vile vile dahamana wakati kesi inaletwa mahakamani( bail pending trial) na hata dhamana endapo utapatikana na hatia ( bail pending appeal).
Tatizo lingine ni bunge, awali makosa amabayo yalikuwa hayana dhamana yalikuwa mauaji na uhaini lakini sasa hivi tunaona wigo wa makosa yasioyo dhamana umeongozeka kamavile wizi wa kutumia silaha, makosa ya kujamiiana, wizi wa fedha ambapo ili kupata dhamana lazima uweke nusu ya hela ambayo imedhaniwa imeibiwa.
Tukiangaliana sana vifungu vinavyozuia dhamana vinakinzana na katiba na sheria inatamka wazi kuwa katiba ni sheria mama, hivyo ni juu yetu kuiomba mahakama kutengua vifungu ambavyo vinakinzana na katiba. Mpaka leo ni watu wachache wamekuwa na ujasiri wa kufanya hivyo.