Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Serikali ya Equatorial Guinea imeminya Mtandao wa Whatsapp Nchini humo ili Raia wake wasiweze kupakua (ku-download) na kusambaza picha pamoja na video kwa kutumia Whatsapp, kufuatia kashfa ya ngono inayomuhusisha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kitaifa la Uchunguzi wa Fedha Nchini humo, Baltasar Engonga ambaye ameingia kwenye kashfa ya kujirekodi akifanya mapenzi na Wanawake zaidi ya 400 Ofisini na nyumbani.
Watumiaji wengi wa Whatsapp Nchini humo wamechukizwa na maamuzi hayo ya Serikali na wengine wamenukuliwa wakilaumu kwamba makosa ya Watu wachache yamefanya washindwe kuendelea na shughuli zao za kawaida kwenye mtandao huo.
Sakata hili la video za ngono kwa Mkurugenzi huyo lilifichuka baada ya upekuzi wa Polisi uliofanywa nyumbani kwake na Ofisini kwake juu ya tuhuma za ufisadi na ulaghai ambapo CD kadhaa zilikutwa zikiwa na video za Wanawake hao zaidi ya 400 wakiwemo Wake za Watu, Mke wa Mchungaji wake Baltasar, Mdogo wake na Rais wa Nchi hiyo pamoja na Wake za Mawaziri zaidi ya 20.