Gumzo la Mohamed Ghassani: Abdul sykes kutoka Burma Infantry 1945 hadi kuunda TANU 1954

Gumzo la Mohamed Ghassani: Abdul sykes kutoka Burma Infantry 1945 hadi kuunda TANU 1954

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
GUMZO LA HARITH GHASSANI: MOHAMED SAID ANAMWELEZA ABDUL SYKES KUTOKEA BURMA INFANTRY 1945, DOCKWORKERS UNION 1949 HADI TAA 1950 NA KUUNDA CHAMA CHA TANU 1954

Baada ya Kipindi Cha Kwanza nilichomzungumza Kleist Sykes fuatilia Kipindi cha Pili namzungumza Abdulwahid Kleist Sykes.

Fuatilia ukurasa huu usikilize historia ya siasa kama zilivyokuwa katika mji wa Dar es Salaam baada ya Vita Vya Pili Vya Dunia.

Yaliyowakuta Waingereza mikononi kwa makuli wa Bandari ya Dar es Salaam mwaka wa 1950 katika maandamano ya kupinga dhulma za serikali ya kikoloni na watalamizi wao hawakuyategemea.

Mambo yalianza baada ya dua na Halal Badr kusomwa Shambani kwa Mohamed Abeid Bonde la Msimbazi watu wakalishana yamini kujikinga na wasaliti.

Makuli wa Bandari ya Dar es Salaam walimwaga katika mitaa ya Dar es Salaam damu zao na za askari Kavirondo Waafrika wenzao waliokuwa wanajiona wao ni sehemu ya mtawala dhalimu.

Yaliyowafika Waingereza kutoka vichwa vya vijana wasomi wa wakati ule waliotokea Makerere tena madaktari wa binadamu, Dr. Vedasto Kyaruzi, Dr. Luciano Tsere, Dr. Wilbard Mwanjisi kuwataja wachache, hayakupata kuwapitia Waingereza hata kwa mbali sana.

In Shaa Allah nitakusomea haya yote kutoka kumbukumbu za wale waliokuwapo wakati ule na kuyaona haya yote kwa macho yao na kuyasikia kwa masikio yao mawili.

Si kweli kuwa uhuru wa Tanganyika ulikuja bila ya kumwaga damu.

1615566534900.png

Dr. Luciano Tsere (1916 - 1970)


20200816_204742.jpg

Abdulwahid Sykes (1924 - 1968)
 
Back
Top Bottom