Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MOHAMED NA MOHAMED SOMO NA SOMO: GUMZO LA MOHAMED GHASSANI
Huwezi kuchoka kumsoma wala huwezi kuchoka kumsikiliza Mohamed Ghassani.
Kipindi chake ''Gumzo la Mohamed Ghassani'' kina wafuatiliaji wengi wakimsikiliza akieleza historia yetu kwa mtazamo tofauti kabisa wa ule uliozoeleka wa kuisomesha historia kutokana na historia rasmi.
Fuatilia ukurasa huu usikilize mahojiano aliyonifanyia somo yangu akitaka nimueleze chimbuko la siasa za ukombozi wa Tanganyika kama mimi nilivyopokea kutoka kwa wazee wangu walioishi Dar es Salaam ya karne ya 19 na kutoka katika tafiti nilizofanya.
Somo yangu ametaka nimrudishe nyuma sana karne ya 19 nimueleze historia ya wazalendo wa nyakati hizo ambao alama zao tunaweza kuziona hivi leo karne ya 21 sasa zaidi ya miaka 100.
Nimemchagulia somo yangu Kleist Abdallah Sykes ambae alizaliwa karne ya 19, yeye mwenyewe kaacha mswada alioandika kabla ya kufariki katika karne ya 20.
Karne ya 20 mwaka wa 1968 Kleist Sykes alikuwa tayari yuko ndani ya Maktaba ya University of East Africa, East Africana akisomwa ndani ya Seminar Paper Idara ya Historia iliyoandikwa na mjukuu wake Aisha ''Daisy'' Sykes na mwaka wa 1973 alikuwa ndani ya kitabu alichohariri John Iliffe, ''Modern Tanzanians.''
Karne ya 21 mradi wa Harvard na Oxford University Press wa kuandika wasifu wa watu mashuhuri Afrika walimtia katika kamusi maarufu kwa jina la Dictionary of African Biography (DAB) ( 2011) yenye volume 6.
Usikose In Shaa Allah kupita hapa kuangalia kipindi hicho.
Image may contain: 1 person, sitting