Gurudumu lisilo tumia upepo

Gurudumu lisilo tumia upepo

chinekeeee

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2015
Posts
1,787
Reaction score
2,894
Kampuni ya Japan yasainifu tairi lisilohitaji kuingizwa upepo.
fa3e26a4-887d-453a-897e-50f5801e2a75_1000.jpg

Kampuni ya mpira ya Toyo ya Japan imesanifu tairi lisilohitaji kuingizwa upepo, na imepata mafanikio katika kuongeza maisha na usalama wa tairi na kupunguza kelele zilizotolewa na tairi wakati gari linapoendeshwa. Kabla ya hapo, makampuni mengine yaliwahi kusaini matairi ya aina hiyo, lakini hayatumiwi kwa wingi kutokana na tatizo la kelele.

Kampuni hiyo inafahamisha kwamba tairi jipya limepewa jina la "No Air", ambalo litatumiwa kwenye gari la kawaida. Tairi hili lina kipenyo cha sentimita 53 na upana wa sentimita 14. Sehemu ya nje ya tairi inatengenezwa na mpira, na ndani inatengenezwa na rasilimali za mseto zinazoimarishwa kwa nyuzi za Carbon. Ndani ya tairi hili pia kuna njiti 100 za utomvu, ambazo zinasaidia kupunguza shinikizo la tairi na kelele zinazotolewa na tairi.

Likilinganishwa na tairi la kawaida linalohitaji kuingizwa hewa, tairi jipya lina maisha marefu, linapozunguka linakabiliwa na vizuizi vichache, na linaweza kusimamishwa ndani ya muda mfupi wakati dereva anapofunga breki.

Kampuni hiyo inasema tairi hili bado lina dosari chache na itaendelea kuliboresha.

sent from iPhone x
 
sisi acha tuendelee kubishana nani kalipa nauli ya ndege
 
Duh...that's great tho. Maana gharama za kujaza upepo zitapungua.
 
Haya maisha itafika hatua kilimo kilichokuwa kinadhalaulika ndipo patakapokuwa kimbilio sasa, maaana waziba pancha, upepo hakuna kazi apo abadae
 
Lina tofauti na gurudumu la kwenye toroli?
 
na waziba pancha na kujaza upepo watapangiwa kaz nyingne.
Sio wote watakaokuwa nayo.
Now days wengi wana smartfon lakini,haimaanishi vitochi na chaja za kobe hakuna..[emoji2] [emoji2]
 
Sio wote watakaokuwa nayo.
Now days wengi wana smartfon lakini,haimaanishi vitochi na chaja za kobe hakuna..[emoji2] [emoji2]
duh lkn kwa hili sdhan labda bei iwe juu sana kwa hiz tires.hv unajua ni ajali ngap kwa mwaka znatokea kwa matair kupasuka?,hv unajua ni watu wangapi wanalala porini kwaajili ya pancha?
 
duh lkn kwa hili sdhan labda bei iwe juu sana kwa hiz tires.hv unajua ni ajali ngap kwa mwaka znatokea kwa matair kupasuka?,hv unajua ni watu wangapi wanalala porini kwaajili ya pancha?
Hata zilivyokuja tubeless tyres watu waliogopa kuwa zingeleta ajali sana, na pia zingekuwa ghali sana. Leo hii kila mtu anatumia tairi zisizo na tube ndani.

Huwezi kuikimbia teknolojia, utaitafuta popote ili uendani na wakati.
 
Back
Top Bottom