PreGE2025 Gwajima anamaanisha kweli kupambana na utekaji au anatafuta ushujaa mitandaoni?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Ungefupisha umeandika sana mpk kusoma kazi. Gwajima yuko sahihi
 
Nimesoma hoja zako, nakushauri uandae press ujitokeze umjibu, na yeye amesema akijibiwa atarudi tena kwa mambo makubwa.

Jitokeze akujibu wewe. Alicho kifanya Gwajima kutumia njia ambayo wewe unasema siyo sahihi, still na wewe njia unayotumia apa siyo sahihi, jitokeze tu kwenye press atakujibu mkuu.
 
Hahahah!! Dk. Gwajima bishop mkuu endelea tulijua na tunajua wametangulizwa machawa wapime kina ss zamisha KABISA mpk mfunga mbwa nae apagawe!!
CHAMWINO na magogoni kwa sasa limekua pango la wezi n mafisadi tu.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Mwandishi ni kama mlevi fulani hivi maswali yote anayouliza majibu yake anayo. Hivi kwa bunge hili ambalo linaongozwa na chawa Tulia Ackson na lililojaa wabunge vilaza ambao huchukua nusu ya muda wao kuchangia kwa kumsifia Samia unategemea lijadili hoja za Gwajima? Spika chawa huyu mara kadhaa amekataa kata kata kupokea hoja za wabunge wanaotaka bunge lijadili utekaji. Hata vikao vya CCM hii ambayo inamuona Samia ni Mungu wao vinaweza kujadili hoja ambayo moja kwa moja inamnyooshea kidole mungu wao? Gwajima yuko sahihi kuliketa suala la utekaji kwenye bunge la wananchi.
 

Hoteli ya nyota 5 anachukuliwa mtu (Boniphace Mwangi)na watekaji wasijulikane mbele CCTV kamera za HD na hao watekaji wasikamatwe mpaka leo inaingia akilini kweli?
Nani yupo salama ndani ya nchi hii kama wahalifu wanawafuata watu ndani ya Hotel ya Nyota 5?
 
Wewe unajua kusoma na kuandika na pengine una akili fulani lakini hujasoma between the lines na pengine unakosa kumbukumbu muhimu kuhusu Bunge na Serikali.

Kwanza, ni kweli asilimia kubwa ya watu wanao tekwa ni wale wanao ikosoa serikali Kwa mapungufu yake na wengine wengine wachache wanao pishana kimtazamo na wenye mamlaka. Hapa ndio maana GWAJIMA amesema siyo kila kosa mtu anastahili kutekwa , kuteswa na kuuawa au kupotezwa kabisa.

Bunge limepoteza mwelekeo! Speaker wa Bunge ni ama hajui majukumu ya Bunge au Bunge na Serikali wameingia ubia. Kwa maneno yake Speaker alisema hawezi kuruhusu mjadala kama huo Bungeni wakati Hana uhakika kuwa watekaji ni nani hasa na kwamba inawezekana hao watu wapo mahali fulani ndani ya Nchi ...! Akili ya kitoto kabisa, ndio utegemee GWAJIMA angepewa fursa hiyo Bungeni?

Ukiwa umemsoma vizuri utagundua kuwa hao wakuu wa Vyombo pengine wamemuomba yeye GWAJIMA amwage mchele hadharani....! Kwasababu wao hawawezi kujisemea! Huo ndio ukweli.Wanasiasa wanatumia udhaifu huo kujinufaisha na kutumia vyombo Kwa manufaa binafsi.

Kuwatumia Polisi kuiba kura ni matumizi mabaya ya Vyombo.

Kuwatumia usalama wa Taifa kuteka na kuwaua wapinzani au kupandikiza vyama ambavyo ni CCM B ni matumizi mabaya ya Vyombo.

Watanzania tunajua jinsi watanzania tunavyo ibiwa na Hawa wana siasa wajinga, sasa dawa ni kupata watu kama GWAJIMA wengi ili wanasiasa wafike mahali wawe WAZALENDO Kwa Nchi yao .

No reforms no election.
 
Nina wasi wasi kama mtoa mada hii si miongoni mwa watekaji. Kwanza ungemuuliza umri wake uenda bado mdogo hajui bunge linavyo endeshwa.

Kwa mtu mwenye akili za kichwani hawezi kumpinga gwajima alichokisema. Uenda akili zake ni za matakoni kama nyuki au mbu. Ndio maana hana uweza kuchambua speech ya Gwajima.
 
Josephat katoa mawazo yake Kama mtanzania, hapigani vita yoyote, ni mawazo tu, yanaweza kuwa mema au mabaya, na wewe toa ya kwako.

Hivi kwenye kikao hapo Dodoma yupo kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…