Gwajima siyo Kibwetere ni mfuasi wa Kibwetere aliyenusurika

Gwajima siyo Kibwetere ni mfuasi wa Kibwetere aliyenusurika

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Wafuasi wa Kibwetere wamegawanyika makundi mawili, wapo wanaotaka kujifanya wanathamini afya zao na kwamba Kibwetere ailiwapotosha au walijua kabisa kwamba Kibwetere anawapotosha lakini kwakuwa walimdharau Mungu wakamthamini Kibwetere Basi kila alichofanya walimpigia makofi. Alipowaambia wafunge macho walifunga na alipowaambia wasujudi walisujudu.

Siku Kibwetere anaondoka Duniani na baada yakuchoma hekalu na kuwapoteza wengi waliomzunguka, ndipo wale walionusurika walipojitokeza nakuanza kumpinga wakiamini hatorudi Tena. Badala wawapongoze wale waliompinga Kibwetere akiwa hai wameendelea kupambana nao na kuwatia ndani waasisi wa vuguvugu lakumpinga.

Gwajima wa Kawe (nachelea kukubali Ni Mchungaji wa kweli) amebaki kumtetea Kibwetere akiamini ipo siku atarejea Duniani. Amebaki kupingana na Ulimwengu na anachofanya Sasa nikutafuta wafuasi ili awatie Moto Kama alivyofanya Kibwetere Senior. Ni kweli amejizolea waumini na atawachoma Moto maana waamini wake wameshindwa kupiga goti nakuhojiana na Mungu wanasubiri Gwajima ndiye aombe kwa niaba yao na Kisha awape maono. Nawakumbusha waumini, Gwajima anachokifanya nikuimarisha misingi iliyowekwa na Kibwetere ili wafuasi wengi waungue kwa Moto kwa maono yake anayoamini na kuwaaminisha watu kwamba ni maono kutoka Mbinguni.

Kwenye hii Vita si Vita yakuelekezwa kwa amri ni Vita yakuomba upewe ufunuo uchanje au usichanje maana hata mwisho wetu hapa Duniani hautotokana na Uvico tu Bali utaendelea kuhusianishwa na ajali, maradhi, sumu nk. Tukumbuke wapo vichaa awajawahi kuchukua taadhari na haukuna ambaye amewahi kututhibitishia kwamba wameathirika kiasi gani, tunawaona wapo kwenye maeneo yao kila siku, means anayewalinda Ni Mungu maana anajua sisi wenye akili timamu atupo tayari kuwawazia.
 
Gwajima ashamaliza mbna mnaendelea kupambana na kivuli chake wazee, na mapokezi yake kitaa ni makubwa Sana , namshaur akae kimya msije mkamuua kama mlivyofanya Kwa jiwe! Watachanjwa tu wale ambao itawalazimu kufanya hvyo ili upate vitu fulani fulani!
 
Gwajiboy yupo sawa kabisa si chanji chanjo na ntaishi Imani nimsingi wa kila kitu
 
Askofu kibwetere ktk hili covid yuko sahihi, ni upumbavu kama nchi kuwekeza nguvu nyingi na Mali ktk vijimafua visivyoweza kuua hata kifaranga cha kuku
 
Kwakiswahiki hii formu inasemaje yoyote anayejua kibeberu anisaidie nataka kuchoma chanjo nimekwama sieliwi kibeberu kabisa
96FC46D7-51CC-413A-8E4A-01A3E1BE0770.jpeg
 
Askofu kibwetere ktk hili covid yuko sahihi, ni upumbavu kama nchi kuwekeza nguvu nyingi na Mali ktk vijimafua visivyoweza kuua hata kifaranga cha kuku
Akili za kuambiwa changanya na zako.
 
Wewe Kama umetumwa tumika tu hutupati,kipi kipya alichosema Gwajima,nabii Loringa aliystabiri kifo Cha JPM,alionya viongozi juu ya chanjo,JPM mwenyewe alionya.

Labda wewe tuthibishie mtu akichanjwa hataugua Tena?

Ni nchi gani ipo salama kwa sababu watu wake wamechanjwa?

Tueleze long term side effects za hiyo chanjo ya Corona. Kama wewe ni mtaalamu,au ni chuki zako na njaa yako.
 
Kwakiswahiki hii formu inasemaje yoyote anayejua kibeberu anisaidie nataka kuchoma chanjo nimekwama sieliwi kibeberu kabisaView attachment 1872422
WauIize Waliowahi kufanyiwa upasuaji, wanaelewa hili, kabla ya kuingia theatre lazima uanguke saini. Hii ni fomu ya KIAPO na serikali haitahusika na athari zozote zitakazokukumba baada ya kuchanjwa.
 
Tutapoanza kuwabeba kuwaweka na kuwatoa juani mkiwa mshakuwa mazezeta ndo mtajua hamjui.
 
Gwajima ashamaliza mbna mnaendelea kupambana na kivuli chake wazee, na mapokezi yake kitaa ni makubwa Sana , namshaur akae kimya msije mkamuua kama mlivyofanya Kwa jiwe! Watachanjwa tu wale ambao itawalazimu kufanya hvyo ili upate vitu fulani fulani!
....jiwe kaenda na covid-19 kwa ubishi wake
 
Back
Top Bottom