Gwambina FC 0-1 Simba SC | Simba yapaa kileleni

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania VPL kupigwa leo Aprili 24, 2021 kwenye Dimba la Gwambina Complex ambapo wenyeji Gwambina FC wanacheza na Mnyama Mkali Mwituni Simba SC.

Simba SC ina nafasi ya kurejea kwenye msimamo wa VPL, endapo tu watashinda mchezo wa leo dhidi ya Gwambina FC huku Gwambina FC wakitamba kuizuia Simba SC kuondoka na alama tutu.

Kocha wa Gwambina FC Mohamed Badru amesema "Tutaizuia Simba SC kuondoka na alama tutu muhimu, tumepoteza mechi mbili zilizopita ugenini lakini tunarudi nyumbani na morali hivyo tutacheza kwa kuwaheshimu ili kuwapa ugumu wa kufunguka na kufanya wanachotaka". Amesema Badru.

Kocha Msaidizi wa Simba SC Suleiman Matola amesema "Haitakuwa mechi rahisi kwasababu mzunguko wa pili kila timu inapambana ili kukaa sehemu nzuri.

Kwahivyo tumejipanga kuhakikisha tunapata matokeo ya ushindi ili tukae kwenye nafasi ya kwanza ya msimamo wa Ligi Kuu". Amesema Matola.

Kumbuka mtanange huu ni kuanzia saa 10: 00 jioni. Usikose Ukasimuliwa

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana.

======

Naaaam mpira umeanza uwanja wa Gwambina Complex, VPL kuwania alama tatu muhimu kwa kila timu

Gwambina FC 0-0 Simba SC.

05' mpira umeanza kwa kasi huku kila timu inapambana kwa mashambulizi ili kupata wala bao la kuongoza huku Gwambina FC wakikosa nafasi moja ya kufunga goli.

15' Bado milango ni migumu kwa pande zote mbili, pamoja na mashambulizi lakini mabeki wa timu zote wamekaa imara.

22' Bocco anakosa nafasi ya kufunga ambapo golikipa anacheza mpira ule.

28' Hussein Goooooooooooooaal Gooooal

Mohamed Hussein anaipatia Simba SC bao la kwanza kwa shutiiiiii kali

Gwambina FC 0-1 Simba SC

Gwambina FC wamepania sana hii game huku Simba SC ikidhamiria kupata ushindi kwa leo.

45+2' kuelekea kuwa mapumziko uwanja wa Gwambina Complex, VPL

Alijaribu mchezaji jezi namba 14 wa Gwambina FC, lakini shuti lake linatoka nje na kuwa Goal Kick

Naaaam mpira ni mapumziko ambapo Simba SC wapo mbele kwa bao moja kwa bila dhidi ya Gwambina FC

HT, VPL; Gwambina FC 0-1 Simba SC

Kipindi cha pili kimeanza uwanja wa Gwambina Complex

Mchuano ni mkali sana kuwania alama tatu muhimu. Wanaume hawa wanapambana.

61' Ametoka Morrison na nafasi yake imechukuliwa na Dilunga upande wa Simba SC

70' Ametoka Saleh na ameingia Rajabu upande wa Gwambina FC, huku Simba wakimtoa Bocco na ameingia Kope Mutshimba Mugalu

Gwambina FC 0-1 Simba SC

78' Onyango anaruka juu anagonga kichwaaa Gooooal. Refaa anakataa bao.

85' Ametoka Kagere na ameingia Mkude upande wa Simba SC, wakati huo huo kuna shabiki ameingia uwanjani lakini Askari wamemdhibiti

90+4' kuelekea kumalizika kwa mchezo.

Naaaam mpira umekwishaaa ambapo Simba SC wameibuka na ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya Gwambina FC bao la Mohamed Hussein dakika 28'

Kwa ushindi huo Simba SC inaongoza kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania kwa alama 58.

FT, VPL; Gwambina FC 0-1 Simba SC
 
Naaaam mpira umeanza uwanja wa Gwambina Complex

Gwambina FC Vs Simba SC
 
Naaammm naaaammm

Usiku wa deni haukawii kukucha

Hatimaye ile siku ya mnyama kuchukua nafasi yake stahiki imewadia

#SIMBA NGUVU MOJA [emoji1491]

Muhimu alama tatu kuendeleza back to back
 
Leo naona Konde Boy hata sub hayupo viwanja vibovu haviwezi. Pia leo wameanza Wote Boko na Kagere.

Kila la kheri mnyama. Kama utopolo waliwafunga Gwambina goli 3, Leo naziona 5
 
Mtoto halali na pesa, watapigwa iwe isiwe na Leo lazima Mnyama akae Kileleni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…