H.E.S.L.B kumbukeni vijana wanawategemea.

Molembe

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
9,917
Reaction score
11,801
Mpaka sasa idadi kubwa ya first year hawajaenda kuripoti kwenye vyuo vilivyoanza usajili kutokana na kutojua hatma yao ya kupata mkopo, hivyo tunaomba bodi mjipange mapema kwa kutoa majina ili muweze kuwatoa wasiwasi vijana wanaotoka familia maskini.
 
Ambao hawajapata mkopo wajilipie. Wafanye harambee. Harambee isiishie kwenye harusi tu. Shule za sekondari hawana bodi ya mikopo, na wanalipa zaidi ya milioni mbili. Lakini hatujawahi kusikika malalamiko. Wazazi wanalipa. Acheni kudeka. Lipeni. Serikali ielekeze nguvu zake kwenye miundo mbinu na huduma nyingine za kijamii.
 
Ovyo!!!!!!!
 
Ovyo!!!!!!!

Ovyo kuchangia kwenye elimu?? Kwenye harusi na kipa imara sawa? Haya. Tubadilike. Mabadiliko ni mimi na wewe. Mmezoea kukariri utaratibu wa maisha. Maisha yana changamoto na yanahitaji innovation. Subiri serikali iwaletee chakula mezani.

 

Sitaki kuamini kama ilikuwa ni lazima uchangie kwenye uzi huu!!! Hivi unaposema acheni kudeka unataka kutuaminisha kuwa wanaoshindwa kusomeshwa kutokana na ufukara walipenda na wanadeka? Ni kweli ukipiga hesabu ya ada yote kama wewe ulisoma government advanced schools ile Ada inakaribia hata tuition's fee ya course hata moja chuo kikuu? Umeudhi na umechefua sana iwe mwanzo na mwisho!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…