Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Profesa Kabudi alisema wazi, kuwa kwenye ishu ya muungano, wazanzibar mambo yao yako mezani, yako well documented isipokuwa yale ya Tanganyika. Akasema anaogopa siku watanganyika watakaponyanyuka na kudai mambo yao
Humphrey Polepole akasema, Katiba ya Sasa inampa Rais wa sasa madaraka makubwa mno yakiwemo ya teuzi za kila namna hadi kuanzia mawaziri hadi wakurugenzi na akasema Makatibu wakuu wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar wanataka serikali tatu na hata makatibu wakuu wa Serikali ya Muungano walitaka Serikali mbili lakini mambo ya muungano yaongezwe, akaendelea kusema kuwa hata kamati ya Makatibu wakuu wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar walitaka mambo ya Muungano yapunguzwe, Ofisi ya waziri mkuu ilitaka serikali tatu na ofisi ya makamu wa wa rais ambayo ilikuwa na dhamana ya mambo ya kujadili kero za mambo ya muungano ilitaka serikali tatu
Bashiru Ally yeye akasema Katiba ya sasa ya mwaka 1977 haiendani na mazingira ya sasa ya mfumo wa vyama vingi.
Kwa hiyo ninashangaa wale wanaomshambulia Lissu juu ya muungano na kutaka kutengeneza muungano mzuri zaidi usio wa manung'uniko kutoka pande zote mbili
Hata rasimu ya Warioba ilisena wazi kuwa Kwa Muundo wa sasa wa Muungano, mambo hayako clear, je Tanganyika ndo Tanzania yenyewe au ni kitu gani?
Kuna njia moja tu inayoweza kuulinda Muungano, njia yenyewe ni:
Tusiwaingilie wazanzibar mambo yao ya ndani, namna hii watatuheshimu na hawatatuona wakoloni. Ila hii tabia ya kuwachagulia viongozi Dodoma na kuwapandikiza ipo siku zanzibar itarevolt, na ikirevolt itavunja muungano.
Iwapo chuki yao dhidi ya Muungano itakuwa kubwa kuliko chuki yao ya upemba na uunguja, huu muungano hauna future.
Na hii chuki dhidi ya Muungano itasababishwa na tabia zetu za kudhulumu sauti za wananchi wa Zanzibar kwenye kujichagulia viongozi wao wenyewe!
1: Humphrey Polepole
2: Profesa Kabudi