Ha ha haaa! Asanteni waarabu kwa 2 kavu dhidi ya Kenya

Mugabe one

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2016
Posts
2,327
Reaction score
1,683
Nilicheka sana kuona wale jirani zetu wanaojifanya wajuaji wajuaji wakati ni hewa walimimiwa 2 kavu kutoka Algeria.

Kilichonifurahisha ni kufungwa mbili kavu pamoja na kujifanya wajuaji wajuaji tu na kujiona wako juu kwa kila kitu.

Naipongeza sana timu ya Burundi na hata taifa stars wajitahidi tu kujitutumua wasiogope majina ya wachezaji wanaochezea ulaya maana hata sisi tunako kamoja tu ka- Mbwana Samatta.

Ila uongozi wa taifa stars waache kubania ile Pesa ya msosi maana vijana walionekana walikuwa hawajala sijui.

Yangu ni hayo tu asanteni waarabu kwa kuwatoa kamasi wakenya.
 
Aaah...!
Wewe ni shabiki au mshabiki wa mpira..?
 
Piere kakatiwa ticket na wenye timu yao ili akatie nguvu ! ....bado unategemea kuna ushindi hapo? Wanasiasa wanatakiwa walete sera mbadala ambayo itatuletea mafanikio hapo baadae na sio mipango ya zimamoto kama hii na sio kumpeleka Pirre au akina Pierre 1000
 
Huku Pierre!
Kule Steve Nyerere!
 
Nawapongeza sana Algeria kwa kutuzawadia hizo mbili, maana wametuhurumia sana....wacha wafu wazike wafu wao. Li nchi la hovyo hovyo tu..Yule Karia yule aache kuropoka ajifunze kuongozi.
 
Tanzania utafikiri ndo wameanza chekechea kwenye viwango vya mpira, ingawa kenya wamefungwa mpira wao ulikuwa unaonekana, tungeambiwa tu kwamba tunaenda kushiriki siyo kushindana
 
Mwambieni kocha wenu aache ujinga wa kuacha wachezaji wazuri kwenye benchi na kuanzisha wa hovyo mtashinda Sisi wakenya hatana Shaka tunajua tukikutana na nyinyi tunawakalisha mapema Sana
 
ila wakenya walijitahidi sana kusukuma mpira tatizo tu,hawa waarabu wako more exprienced
 
Ni mpumbavu tu anayeweka siasa kwenye michezo labda tu kama anataka kumfurahisha bwana yake.
Moderetazi ondoeni uzi huu wekeni kwenye michezo.
 
Hapa naanza kuona machungu ya kila siku Tanzania kufungwa sisi tuu?, tumegeuzwa kichwa cha mwenda wazimu.
Lakini kwa upande mwingine nachelea kusema ni aina fulani ya ROHO MBAYA WALIYONAYO NDUGU ZETU WA TANGANYIKA DHIDI YA ZANZIBAR(yaani TFF dhidi ya ZFA) pale walipoomba kutambuliwa na FIFA na CAF na kutakiwa wapate saini ya TFF KAMA MDHAMINI WAO kwa vile wao ndio wanaosimama kwa jina la Tanzania (sovereign).

Hivyo hivyo siku ile timu ya Zanzibar ya vijana(Zanzibar Herro) ilipocheza na Bara na kuifunga, wenzetu Bara wakatununia, na siku tulipoingia fainali na Kenya wakahiari kutupikia majungu ili kenya ishinde kulikoni sisi ndugu zao.

Hapa naona jambo la Muungano halikuleta udugu wala mapenzi baina yetu,na ndio maana kila siku wenzetu Bara hujivutia maslahi kwao tuu na hata kusababisha Miradi ya Kiuchumi ya Zanzibar kama Bandari ya Mpiga duri,Uwanja wa Ndege wa Unguja,na Barabara ta wete mkoani ambazo tayari tumesha pata ufadhili, wao watie saini kama mdhami tu kwa vle wao ndio wenye (sovereign) wametukatalia eti wakidai kuwa Bandari ya Mpiga duri itauwa Bandari ya Dar.

HIVI KUMBE ZANZIBAR SI TANZANIA !?
Ndio maana jana nimeona Vijana wa kizanzibari wakiishangilia SENEGAL DHIDI YA TAIFA STAR
Nlishangaa lakini ndio ukweli wenyewe ,unyama unyama tuu, ila hali si nzuri Muungano wetu Uko mahskani
TUJADILI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…