kama umeona serikali imeuza loliondo na watu wanachomewa nyumba hawana pa kukaa na iko kimya?huna haja ya kuongea kuhusu parking ya mengi,inadhuru au kuhusiana vipi na mahitaji ya wananchi?licha ya hivyo MZEE MENGI ni msaada na ni mtu mzuri sana katika kusaidia na kujali ubinadamu unapomfikia,kusema kweli jamani mi kuhusu huyu mzee nampa heshima yake,ni tofauti kabisa na hao watu mnawaita viongozi.kuhusu ufisadi na kilakitu nani si fisadi tanzania?MWACHENI MZEE APUMZIKE,ANA THAWABU NYINGI KULIKO LAANA MNAZOMTUPIA,NA NI MFANO KATIKA JAMII
Wee Mtu vipi? Umeni-quate maneno yangu na hukusoma hata kimoja nilichoandika. Mbona unanipandikiza maneno ambayo mie sikusema? Hebu soma tena ujumbe wangu na urudie tena. Mbona wakimshambulia huwa anakuja kwetu kuanza kulialia? Sasa sisi tunasema kuwa "badala ya kugawa pesa, awe mfano wa kuigwa kwa watu". Awaonyeshe watu jinsi ya kuvua samaki na kugawa ndoano badaya ya samaki (pesa) ambazo siku zote zinalemaza watu.
Ombi langu kwa Mengi ni dogo sana:-
1. Awe mfano kwa kutunza mazingira sehemu anayokaa na anayofanyia kazi.
2. Awe kiongozi kwa kuwaongoza watu kutunza mazingira sehemu wanazokaa.
Nani hapa anaongelea Serikali ya CCM? Ile hamna cha kuongea tena maana tumeongea saana na hakuna kinachoendelea. Kama watu wakianza kupata mwamko wa kubadili maisha yao, itakuwa ni shule nzuri sana ya kufahamu ni kiongozi gani anawafaa kuwaongoza. Tatizo unapoishi sehemu kunanuka vinyeshi (maana mvua ikinyesha watu wanatapisha vyoo) na unakwenda kwa Mengi unakuta hayo maji taka yanapita mbele ya Ofisi yake na yeye kapumzika ndani (na watu kama wewe wanasema tumwache apumzike) unafikiri nitapata shule yoyote? Mengi ni Bench Mark ya Watanzania wengi kuwa kama yeye Mpingo mwenzetu kaweza, basi na sisi tunaweza. Wasukuma wengi sana kwa sasa wanafanya kazi usiku na mchana ili kushindana na Wachaga/Mengi. Kama huyu asingelikuwepo, si na wao wangebweteka? Mengi inabidi aongeze urefu wa eneo la mashindano na ikibidi hata uwanja wa mashindano aubadilishe.
Mengi hawezi kupumzishwa maana UMAARUFU UNA GHARAMA ZAKE.
Halafu hizi HESHIMA unazompa, naona hata akikutia kidole machoni, wala hutaona maana UMESHAKUWA KIPOFU. Mengi ni binadamu tu kama wengine zaidi ya kuwa MASHUHURI, Pesa, kutoa ajira na misaada kibao. Ombi ni kubadilisha tu namna ya kutoa misaada.
UNAFAHAMU KITU HIKI: European Union wanatoa saana misaada kwa nchi members. Ila wote huwa wanaambiwa kitu kimoja. Ukitaka msaada kujenga barabara basi tafuta Euro 1M na sisi tutakupa 3M. Kama huwezi kupata hiyo 1 Euro, hizo 3 Euro huzipati. Hapo watu huchakalika saana ili kukusanya Euro za kutosha kupata 3 zaidi katika kila moja. Ila wakija Afrika (na Mengi anafanya hivyo) wala hawaweki masharti..... chukua tu mwanangu ukaolee mke wa pili. Misaada, My A**.