Jospina
JF-Expert Member
- Apr 19, 2013
- 2,421
- 1,395
Naomba mnisaidie kuwarekebisha jamaa hawa. Wahenga walisema HABA NA HABA HUJAZA KIBABA. Kamwe, katu, katiti, abadan wahenga hawakusema "haba na haba hujaza KIBUBU". Hapana, tusiwalishe maneno wahenga wetu.Naomba waambieni hawa jamaa waseme hivi; "Wahenga walisema haba na haba hujaza KIBABA lakini sisi tunasema haba na haba hujaza KIBUBU". Watoto wetu shuleni wakiulizwa kujaza methali ya haba na haba.... kuna hatari wakajaza "hujaza kibubu" Baraza la Kiswahili la Taifa mko wapi?